Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

4 0 /

U O N G O F U & W I T O

uliyoagizwa na uandike muhtasari usiozidi aya moja au mbili kwa kila eneo moja. Katika muhtasari huu tafadhali toa uelewa wako bora zaidi wa kile unachofikiri kilikuwa jambo kuu katika kila eneo husika la usomaji. Huhitaji kutoa maelezo mengi; andika tu kile unachoona kuwa jambo kuu linalozungumziwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali kabidhi muhtasari huo darasani wiki ijayo. (Tafadhali ona “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” kwenye ukurasa wa 16). Katika somo la juma lijalo tutaendelea kuchunguza nguvu za Neno la Mungu kama chombo cha Roho Mtakatifu ili kuuthibitishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki, na hukumu. Kuhusu dhambi, Neno hututhibitishia kuhusu kutotii sheria ya Mungu na kutotii kwetu. Kuhusu haki, linamdhihirisha Bwana kuwa mwenye haki isiyo na kikomo na haki yetu wenyewe kuwa haikubaliki. Kuhusu hukumu, linaonyesha nia ya Mungu kuhukumu viumbe vyote kwa msingi wa vigezo vya haki yake, na utii wao kwa vigezo hivyo. Pia tutaona jinsi Neno linavyotuthibitishia juu ya kweli ya Yesu Kristo kama mada kuu na lengo kuu la Biblia, Ufalme wa Mungu kama msingi wa hadithi ya Mungu, manabii na Mitume kama mashahidi wa kweli na wa kutegemewa wa ufunuo wa Mungu ulimwenguni.

Kuelekea Somo Linalofuata

1

Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia nyenzo hizi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali tafuta uthibitisho wa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license.

Made with FlippingBook flipbook maker