https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 3 2 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

• Ingawa Maandiko yanahusianisha mji wa Yerusalemu na uasi wa wanadamu, yanafundisha pia kwamba Mungu aliukubali mji huo kuwa ishara ya makao yake na baraka zake. Licha ya ukweli kwamba Daudi aliushinda mji huo kwa njia ya vita, Mungu aliuchagua Yerusalemu kwa ajili yake mwenyewe, na akaamua kuufanya kuwa wenye sifa duniani. Ajabu ya Kimungu ni hii hapa: Mungu anabadilisha taswira ya kidunia ya “kujitegemea na uasi” kuwa taswira ya “ kimbilio ” (k.m. miji ya makimbilio), na picha ya upatanisho , mahali pa kuujua na kuupata msamaha na baraka zake (k.m. Yona na kisa cha Ninawi). • Kwa sababu ya rehema na neema ya Mwenyezi Mungu katika Kristo, tumaini lipo kwa mji wowote unaotubu mbele ya hukumu yake, unaojinyenyekeza chini ya matakwa yake, na kutafuta rehema zake mbele ya adhabu yake. Kwa hiyo, mapema kabisa kitabu cha Mwanzo kinaweka mtazamo wa jumla wa ulimwengu ambao taswira ya mji ni hali ya kumpinga Mungu, ambayo inajaribu kuzuia utawala wa Mungu juu ya ulimwengu. Ni mahali ambapo utamaduni unapindua dini kwa makusudi yake badala ya kuendeleza utukufu wa Mungu. Kitabu cha Mwanzo kinatoa usuli huu kwa Waisraeli walioishi katikati ya uumbaji usio na maana, mada iliyoendelezwa katika simulizi ya kitabu cha Kutoka ya utumwa wa kukandamiza wa Israeli na kutumikishwa katika mpango wa ujenzi wa jiji la Misri (Kut. 1:8-14; 5:5-21). Kusudi la asili la Mungu kwa ajili ya wanadamu wenye sura na mfano wake lilikuwa kujenga jamii kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Walipaswa kuongezeka na kuenea juu ya dunia, kupanua utawala wa Mungu juu ya viumbe kama watawala wasaidizi wa Mungu (Mwa. 1:26-28). Kwa sababu walitumia uhuru [kujitegemea bila Mungu], mwanamume na mwanamke wa kwanza walilaaniwa na kufukuzwa kutoka katika uwepo wa Mungu ili kungojea utimilifu wa ahadi ya Mungu ya kuwakomboa kutoka chini ya laana hiyo (Mwa. 3, msisitizo katika mst. 15 na 24). Juhudi zote katika ujenzi wa jiji kuanzia hatua hiyo na kuendelea ni uthibitisho wa uhuru huo wa asili. ~ Leland Ryken . The Dictionary of Biblical Imagery. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 151. Jiji kama Ishara ya Uhuru na Uasi

I. Misingi ya Kibiblia: Kufafanua Jiji

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

3

Made with FlippingBook Annual report maker