https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 1 5 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
c. Miji ya viwanda (miji yenye kelele na shughuli nyingi za uzalishaji wa viwandani) k.m., Bombay, Sao Paulo, eneo la Chicago-Gary.
d. Miji ya kibiashara (masoko na maduka makubwa ambapo bidhaa na huduma hubadilishwa kwa kiwango cha kimataifa) k.m., New York, Hong Kong.
e. Miji ya alama au ya kihistoria (miji ambayo mapambano makubwa yanapiganwa na kutatuliwa na kuwekewa alama ya kumbukumbu, au ambayo inawakilisha masuala ya migawanyiko, ukandamizaji, vita, chuki ya kidini, au uhuru ndani ya nchi zao au kwa ulimwengu wote) k.m., Soweto, Belfast, Berlin, Beirut, Jerusalem.
f. Miji ya msingi (miji ambayo inachanganya sifa zote zilizotangulia, na inaweza kusemekana kuwa miji mikuu zaidi) k.m., Bangkok, Mexico City, London.
3
3. Wakazi wengi wa mijini wanaishi wapi? Miji kumi na mitano yenye mikusanyiko mikubwa zaidi ya watu, iliyoorodheshwa kwa msingi wa ukubwa wa idadi ya watu kufikia 2015. Hivi sasa, miji kumi na miwili mikubwa iko Asia, mitatu Amerika Kusini, miwili Marekani na mmoja barani Afrika (Matarajio ya Ukuaji wa Miji Duniani; Marekebisho ya 1996. New York: Umoja wa Mataifa, 1998) [idadi ya watu kufikia 1998].
a. Tokyo, Japani 28.9
b. Bombay, India 26.2
c. Lagos, Nigeria 24.6
Made with FlippingBook Annual report maker