https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
1 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika moduli hii ya Capstone iitwayo Misingi ya Utume wa Kikristo , utahitajika kufanya ufafanuzi (uchambuzi wa kina) wa mojawapo ya vifungu vifuatavyo vya Neno la Mungu kuhusu asili ya utume wa Kikristo na huduma ya mjini: Mathayo 28:18-20 2 Wakorintho 6:1-10 Luka 4:16-22 2 Timotheo 4:1-5 Mathayo 5:13-16 Wakolosai 1:24-29 Madhumuni ya kazi hii ya ufafanuzi wa Maandiko ni kukupa fursa ya kufanya utafiti wa kina wa kifungu kimojawapo muhimu kuhusu asili na utendaji wa utume wa Kikristo. Kuona kwamba Mungu ni Mungu wa umisheni ni jambo la msingi kwa kila hatua ya huduma ya mjini; umisheni sio msisitizo wa msimu fulani wala kazi ya watu wachache wasio wa kawaida walio tayari kwenda ng’ambo kwa muda. Umisheni (utume), badala yake, ndio damu au kiini cha mtazamo wa ulimwengu wa Kiyahudi-Kikristo, moyo na roho ya utendaji wa Mungu duniani. Kwa maana moja, hadithi nzima ya Kikristo inaweza kuelezewa kama nia ya Mungu ya kuvuta kutoka duniani watu ambao watakuwa mali yake; umisheni ni kazi ya Mungu na kazi yetu. Madhumuni ya utafiti huu ni ili uweze kuchagua mojawapo ya maandiko hapo juu na kulitumia kama lenzi ambayo unaweza kuitumia kutafakari na kufikiria kwa kina kuhusu umisheni – msingi wake, utendaji wake, na umuhimu wake kwa uongozi wa Kikristo wa mijini. Unapojifunza mojawapo ya maandiko haya (au andiko lingine ambalo wewe na Mshauri wako mtakubaliana) tumaini letu ni kwamba utaangazia kipengele muhimu cha msingi wa umisheni wa Kikristo. Pia tunatamani kwamba Roho akupe ufahamu kuhusu jinsi unavyoweza kuhusianisha maana ya andiko hilo moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, na Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)
Dhumuni
Made with FlippingBook Annual report maker