https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

1 7 2 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo ya Utume wa Kikristo na Jiji , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Bakke, Ray, and Jim Hart. The Urban Christian: Effective Ministry in Today’s Urban World. Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1987. Conn, Harvie M., and Manuel Ortiz. Urban Ministry: The Kingdom, the City, and the People of God. Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001. Lupton, Robert D. Theirs Is the Kingdom: Celebrating the Gospel in Urban America. New York: HarperCollins Publishers, 1989. Perkins, John. Restoring At-Risk Communities: Doing It Together and Doing It Right. Grand Rapids: Baker Books, 1995. Kiini cha kazi hii ni kutafuta kuhusianisha kweli hizi kuhusu jiji na jukumu lako kama kiongozi wa kanisa mjini katika huduma yako mwenyewe kupitia kanisa lako. Jinsi Mungu anavyoweza kukutaka ubadilishe au urekebishe mbinu yako ya huduma kulingana na kweli hizi inategemea sana uwezo wako wa kusikia kile ambacho Roho Mtakatifu anakuambia kuhusu mahali ulipo kiroho, kimaisha na kihuduma, uongozi wako wa kichungaji uko katika hali gani, washirika wa kanisa lako wana hali gani, na ni kitu gani hasa ambacho Mungu anakuita kufanya sasa hivi, kama kuna chochote, kuhusu kweli hizi. Panga kutumia muda mzuri wiki hii kutafakari juu ya ajabu ya kiungu ya Mungu kuchagua jiji kama taswira yake ya kimbilio, upatanisho, na urejesho, na ufikirie jinsi huduma yako mwenyewe inavyoweza kubadilishwa kupitia mtazamo huu wa Mungu juu ya umuhimu na nguvu za miji. Unapofikiria kazi yako ya huduma kwa vitendo kwa ajili ya moduli hii, unaweza kuitumia kujumuisha maarifa haya juu ya utume na jiji kwa njia ya vitendo ya moja kwa moja kwa kikundi unachohudumia mara kwa mara. Utafute uso wa Mungu ili kupata ufahamu, na urudi wiki ijayo tayari kushirikishana ufahamu wako pamoja na wanafunzi wengine katika darasa lako. Daima chukua muda wa kuomba kuhusu masomo yako, hata nyakati zile ambapo inaonekana kwamba hakuna mzigo maalum au ufahamu unaoonekana kushika akili na moyo wako. Nidhamu ya maombi ni muhimu katika kujifunza maarifa ambayo Roho Mtakatifu anatamani kukupa kutokana na kazi ya kiakili uliyoifanya kuyachimbua kutokana na kujifuna kwako katika moduli. Calvin anatoa maoni juu ya hitaji hili la nidhamu katika maombi, bila kujali hisia au miongozo ambayo unaweza kuwa nayo:

Nyenzo na Bibliografia

Kuhusianisha Somo na Huduma

3

Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook Annual report maker