https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
2 1 4 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Hitimisho
» Yesu alijitambulisha kwa ukaribu na maskini, katika wito wake kama Masihi wa Mungu na Kichwa cha Kanisa. » Akiwa Mtumishi Atesekaye aliyetimiza unabii wa Kimasihi, Yesu ameunda jamii mpya, Kanisa, ambalo utume wake ni kutangaza Habari Njema ya Ufalme kwa maskini na kujitahidi kuakisi maisha ya Ufalme huo kwa washirika wake na majirani zake. » Mungu atujalie Roho Mtakatifu, Yeye pekee awezaye kufanya shalom kuwa halisi na kweli katikati ya watu wa Mungu leo. Amina.
Kanisa Zima Lihamasishwe Kuchangia Utume, Maadamu Muda Ungalipo
Kanisa zima linahamasishwa kuchangia utume. Kanisa linamwabudu Mungu moja kwa moja (1 Pet. 2:9; Ebr. 12:28, 29; Rum. 15:5-12), linawahudumia watakatifu (Efe. 4:12-16) na ulimwengu (Lk. 24:48; Mdo. 5:32; Flp. 2:14-18). Njia za huduma ni pamoja na: huduma ya neno; huduma ya utaratibu, ambayo kwayo maisha ya Kikristo yanatii sheria ya upendo; na huduma ya rehema, ikidhihirisha huruma ya Kristo. Njia hizi za huduma ni za kawaida kwa waamini wote wanapotafuta kutimiza wito wao. Baadhi ya washirika wa mwili wa Kristo wana karama katika moja au zaidi ya sehemu hizi kwa kiwango kisicho cha kawaida. Kuna karama za kiutawala ambazo zinahitaji kutambuliwa kwa utendaji wake thabiti. Kwa sababu hiyo, Agano Jipya linaelezea ofisi katika kanisa: mitume na manabii kuweka msingi na kuanzisha utume (Efe. 2:20; 3:5); wainjilisti, wachungaji na walimu kutangaza neno lililofunuliwa kwa mamlaka (Efe. 4:11); wengine wenye karama kwa ajili ya maongozi huungana nao katika kuliongoza kanisa (Rum. 12:8; 1Kor. 12:28; 1 T im. 5:17); na mashemasi husimamia huduma ya rehema (1 Tim. 3:8-13). Wale wanaotawala wametolewa na Kristo kwa kanisa kwa kusudi la kulitumikia katika jina lake, chini ya ubwana wake. Nguvu za kanisa ni za kiroho (2 Kor. 10:3-6), kwa ajili ya huduma (1 Pet. 5:3; Mt. 20:25-28), na zinatenda kazi kupitia matamko tu (Mk. 7:8; Ufu. 22:18, 19). Hata hivyo zina mamlaka halali (Mt. 16:19; 18:17-20; 10:14-15; Ebr. 13:17). ~ E. P. Clowney. “Church.” The New Dictionary of Theology. S. B. Ferguson, mh. (toleo la Kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 142.
4
Made with FlippingBook Annual report maker