https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 2 6 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
KIAMBATISHO CHA 18 Orodha Hakiki ya Vipengele vya Simuli Imetolewa kutoka kwa Mtaalamu wa lugha, Profesa Leland Ryken. Namna ya Kusoma Biblia kama Fasihi.
I. Nini Mandhari ya Hadithi?
A. Mazingira yanayozunguka B. Mazingira ya kihistoria C. Hali ya kitamaduni D. Mahusiano kati ya mtu na mtu na mazingira yao
II. Akina nani ni Wahusika katika Hadithi?
A. Akina nani ni wahusika wakuu au wahusika wasaidizi katika hadithi? B. Nani ni “shujaa?” nani ni “adui”? C. Ni kwa namna gani mwandishi anaelezea ukuaji wa muhusika? D. Nini matokeo ya mwisho ya maisha na machaguo ya muhusika?
III. Ni Migogoro Gani ya Kisa husika Iliyopo katika Hadithi?
A. Nini migogoro mikuu na Mungu? B. Nini migogoro mikuu na watu wengine?
C. Nini migogoro mikuu kati ya wahusika wao wenyewe? D. Nini ni migogoro mikuu kati ya wahusika na hali zao?
IV. Ni Vipengele vipi vyenye Mafumbo katika Simulizi ambavyo Vimejifunua kwenye Hadithi? A. Nini kinatushawishi sisi tuweze kupata huruma pamoja na wahusika? B. Nini kinazalisha karaha na chuki kati yetu na wahusika? C. Kwa namna gani tumeandaliwa kuthibitisha kile ambacho wahusika wamefanya? D. Ni matukio gani ambayo yanatufanya sisi tusiwakubali wahusika?
Made with FlippingBook Annual report maker