https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 3 5 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Jinsi ya KUPANDA Kanisa (muendelezo)

Jinsi ya KUPANDA Kanisa

FANYA MAANDALIZI

Fanya Uinjilisti

• Unda timu ya kupanda kanisa. • Omba. • Chagua eneo na jamii lengwa. • Fanya utafiti wa demografia na ethnografia. ANZA KAZI • Andikisha watenda kazi wa kujitolea na uwape mafunzo. • Endesha matukio ya Injili (mikutano, n.k) na uinjilisti wa nyumba kwa nyumba. KUKUSANYIKA • Anzisha vikundi seli, mafunzo ya Biblia, n.k. kufuatilia waongofu wapya, kuendelea na uinjilisti, na kutambua na kuwafunza viongozi wanaoibuka. • Watangazie majirani kuhusu kuanzishwa kwa kanisa jipya na mkusanyike mara kwa mara kwa ajili ya ibada ya hadhara, mafundisho na ushirika. LEA • Kuza ufuasi wa mtu binafsi na wa kikundi. • Jaza majukumu muhimu katika kanisa: tambua na utumie karama za Roho. KIPINDI CHA MPITO • Hawilisha uongozi kwa viongozi wenyeji ili waweze kujitawala, kujitegemeza na kujizidisha (Teua wazee na wachungaji). • Kamilisha maamuzi kuhusu ushirikiano wa kimadhehebu au ushirikiano na taasisi nyingine. • Lipe kanisa mamlaka ya kujiendesha. • Kuza ushirika na World Impact na makanisa mengine ya mijini kwa ajili ya ushirika, msaada, na huduma ya umisheni.

Andaa

Wezesha

Made with FlippingBook Annual report maker