https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi

/ 4 0 5

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Kushika Imani, Sio Dini (muendelezo)

na kuchukuliwa kama ni wa Kimagharibi ingawa asili yake si Magharibi. Ukristo halisi ni utii, uhusiano, ambao kupitia huo hutiririka mfululizo wa maana zilizokusudiwa kuakisiwa kupitia miundo ya utamaduni wowote. Hivyo basi, miundo hii imekusudiwa kuchaguliwa kwa kufaa kwake ili kuwasilisha maana sahihi za kibiblia katika muktadha wa wapokeaji. Ninaamini Ukristo umekusudiwa kuwa “imani,” sio mkusanyiko wa miundo ya kitamaduni, na kwa hiyo unatofautiana na dini hizo. Dini, kwa sababu ni mambo ya kitamaduni, zinaweza kurithishwa kwa tamaduni mpya. Urithishaji huo ni jambo la nje linalosababisha mabadiliko madogo au makubwa katika mifumo ya dini. Ukristo, hata hivyo, unaweza kuwekwa katika muktadha, mchakato ambao maana zifaazo zinaweza kubebwa katika muundo na mfumo tofauti kabisa ndani ya tamaduni mbalimbali. Kwa bahati mbaya, kwa sababu ya kuingiliwa kwa ukristo wa kitamaduni, hatujaona aina zote za utofauti zinazowezekana…

Made with FlippingBook Annual report maker