https://user-fNLORqa.cld.bz/Misingi-ya-Utume-wa-Kikristo-Mwongozo-wa-Mkufunzi
/ 9 1
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo: Sehemu ya Pili Sehemu ya 2: Utume kama Vita vya Milki
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Taswira ya Utume kama Vita vya Milki labda ndiyo taswira ya utume yenye nguvu zaidi katika Maandiko, na huanza na utawala mkuu wa Mungu Yahweh kama muumbaji na mtegemezaji wa yote. Utawala wa Mungu ulipingwa katika “siri ya kuasi” (yaani, uasi wa kishetani huko mbinguni), ambao ulisababisha majaribu na anguko la wanadamu, na laana kwa uumbaji. Mungu aliweka uadui kati ya Uzao wa mwanamke na nyoka, na kwa ukuu wake na neema yake akaahidi kukomesha uasi huo kupitia Uzao wa mwanamke. Kama matokeo ya Anguko, ulimwengu uko vitani, na Mungu amejitangaza kuwa anapigana na nyoka na wale walio upande wake. Mungu alijidhihirisha kuwa Shujaa wa kiungu katika mapambano yake dhidi ya uovu uliofananishwa na mto na bahari, kushindwa kwa Farao na majeshi yake, na mataifa ya Kanaani. Kwa namna isiyo tarajiwa, Mungu pia alilazimika kupigana na watu wake mwenyewe kwa sababu ya kutotii kwao na uasi wao. Zaidi ya hayo, manabii wa Israeli walimfunua Mungu kama Shujaa wa kiungu ambaye hatimaye kupitia Masihi wake angeharibu uovu wote mara moja, milele. Utawala huu wa Kimasihi umewekwa ndani ya Yesu, ambaye katika kuzaliwa kwake, mafundisho, miujiza, kufukuza pepo, matendo yake, kifo chake, na ufufuo wake ameuleta Ufalme wa Mungu. Ufalme uko “tayari” na “bado;” tayari umekuja kupitia Yesu ambaye ametimiza ahadi ya Kimasihi, lakini utakamilika wakati wa Kuja kwake Mara ya Pili. Leo katika ulimwengu huu na katika zama zetu, Kanisa la Yesu Kristo ni ishara na kionjo cha Ufalme uliopo. Roho Mtakatifu anakaa ndani ya Kanisa kama dhamana (arabuni) ya urithi kamili ujao. Kanisa sasa, kama wakala wa Ufalme na naibu wa Kristo, limepewa mamlaka ya kutangaza na kudhihirisha ushindi wa Kristo dhidi ya Shetani na laana. Umisheni unatangaza kwamba katika zama hizi Mungu anaimarisha utawala wake leo juu ya ulimwengu wake katika Yesu Kristo, na kupitia wakala wake, Kanisa. Lengo letu katika sehemu hii, Utume kama Vita vya Milki , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Taswira ya Utume kama Vita vya Milki pengine ndiyo taswira yenye nguvu zaidi ya utume katika Maandiko, na inahusika moja kwa moja na kuanzishwa na kutangazwa kwa utawala wa ufalme wa Mungu katika Yesu wa Nazareti.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
2
Made with FlippingBook Annual report maker