Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

Akiamini madai ya msingi ya Kikristo kwamba kusudi la Biblia ni kumtambulisha Mwokozi, Geisler anamzingatia Kristo kama umoja na ujumbe unaoendelea wa Maandiko yote. Kristo ndiye kiungo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya, maudhui ya kanoni, na mada unganishi ndani ya kila kitabu cha Biblia. Kitabu hiki ni cha msingi kwa masomo ya Biblia na kuhubiri na kinatumika kama mwongozo bora kwa mada kuu ya Biblia. Kinajumuisha zaidi ya utafiti wa mifano (vivuli) na unabii wa Agano la Kale. Kila sura inachukua kwa uzito uthibitisho wa Yesu: “Ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi” (Luka 24:44). Kuhusiana na msukumo mkuu wa Geisler – kwamba Kristo ndiye ujumbe wa Biblia nzima – ni madai ya wazi kuhusu uvuvio wa Maandiko na uungu wa Kristo. Mada za sura ni pamoja na: (1) Kristo Ndiye Ufunguo wa Biblia; (2) Kristo katika Agano la Kale; (3) Kristo katika Maagano yote Mawili; (4) Kristo katika Kila Sehemu ya Biblia; (5) Neno la Mungu: Neno-Mtu na Neno-Kauli. Pia ni pamoja na bibliografia, faharasa ya mada, na faharasa ya Maandiko. Norman Geisler ni mwandishi na mwandishi-mwenza wa takriban vitabu hamsini na mamia ya makala. Amefundisha katika ngazi ya chuo kikuu na shahada za juu kwa karibu miaka arobaini na amezungumza au kujadiliana katika majimbo yote hamsini ya Marekani na katika nchi ishirini na tano duniani kote. Anayo Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Loyola na sasa anahudumu kama Rais wa Southern Evangelical Seminary, katika mji wa Charlotte, NC.

Ruhusa imetolewa na Norman Geisler kwa TUMI ya World Impact kutafsiri na kuchapisha kitabu hiki, 11/2014.

www.worldimpact.org

Made with FlippingBook Digital Publishing Software