Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
Jiwe Walilolikataa Waashi Limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni
THE UR BAN
Kutafsiri Biblia
MI N I S T R Y I NS T I TUT E h u d uma y a WOR L D IMPAC T , I NC .
Mwongozo wa Mkufunzi
Moduli ya 5 Masomo ya Biblia
SWAHILI
M W O N G O Z O W A M K U F U N Z I
Kutafsiri Biblia
Moduli ya 5
Masomo ya Biblia
Kuvuviwa kwa Biblia:
CHIMBUKO NA MAMLAKA YA BIBLIA
Hemenetiki ya Biblia:
MBINU YA HATUA TATU
Fasihi ya Biblia:
KUTAFSIRI TANZU ZA BIBLIA
Masomo ya Biblia:
KUTUMIA ZANA ZA KUJIUNZIA KATIKA KUJIFUNZA BIBLIA
Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia nyenzo hizi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .
Moduli ya 5 ya Mtaala wa Capstone: Kutafsiri Biblia – Mwongozo wa Mkufunzi. ISBN : 978-1-62932-364-0 © 2005, 2011, 2013, 2015. Taasisi ya The Urban Ministry Institute . Haki zote zimehifadhiwa. Toleo la Kwanza 2005, Toleo la Pili 2011, Toleo la Tatu 2013, Toleo la Nne 2015. © 2023 Toleo la Kiswahili, kimetafsiriwa na Robin Mwenda, Rose Mghwai na Eresh Tchakubuta. Hairuhusiwi kunakili, kusambaza na/au kuuza machapisho haya, au matumizi mengine yoyote pasipo idhini, isipokuwa kwa matumizi yanayo ruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Haki Miliki ya Mwaka 1976 au kwa idhini ya maandishi kutoka kwa mmiliki. Maombi ya idhini yatumwe katika maandishi kwa taasisi ya: The Urban Ministry Institute , 3701 E. 13th Street, Wichita, KS 67208. Taasisi ya The Urban Ministry Institute ni huduma ya World Impact, Inc Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997 na The Bible Society of Tanzania. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.
Yaliyomo
Muhtasari wa Kozi
3 5 7
Kuhusu Mkufunzi
Utangulizi wa Moduli
Mahitaji ya Kozi
15
Somo la 1 Kuvuviwa kwa Biblia: Chimbuko na Mamlaka ya Biblia
1
61
Somo la 2 Hemenetiki ya Biblia: Mbinu ya Hatua Tatu
2
113
Somo la 3 Fasihi ya Biblia: Kutafsiri Tanzu za Biblia
3
169
Somo la 4 Masomo ya Biblia: Kutumia Zana za Kujifunzia katika Kujifunza Biblia
4
221
Viambatisho
299
Kufundisha Mtaala wa Capstone
309
Maelekezo ya Mkufunzi kwa – Somo la 1
317
Maelekezo ya Mkufunzi kwa – Somo la 2
323
Maelekezo ya Mkufunzi kwa – Somo la 3
327
Maelekezo ya Mkufunzi kwa – Somo la 4
/ 3
K U T A F S I R I B I B L I A
Kuhusu Mkufunzi
Mchungaji Dkt. Don L. Davis ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry Institute na ni Makamu wa kwanza wa Rais wa World Impact. Alisoma katika Chuo cha Wheaton College na Chuo cha Uzamili cha Wheaton na kuhitimu kwa ufaulu wa kiwango cha juu, yaani Summa Cum Claude, katika ngazi ya Shahada (1988) na Shahada ya Uzamili (1989) katika Masomo ya Biblia na Theolojia ya Utaratibu. Alipata Shahada yake ya Uzamivu katika Masuala ya Dini (Theolojia na Maadili) katika chuo kikuu cha Iowa School of Religion. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi na Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact , anasimamia mafunzo ya wamishonari wa mijini, wapanda makanisa, na wachungaji wamajiji, na kufanya uwezeshaji kupitia fursa zamafunzo kwa watendakazi Wakristo wa mijini katika uinjilisti, ukuaji wa kanisa, na umisheni wa upainia. Pia anaongoza Mpango wa Mafunzo huria kwa wale wanaosoma wakiwa mbali, vilevile anawezesha Mafunzo ya Kiuongozi kwa mashirika na madhehebu kadhaa kama Prison fellowship, The Evangelical Free Church of America na The Church of God in Christ. Dkt. Davis, ambaye ametunukiwa tuzo nyingi za ualimu na za kitaalamu, amewahi kuwa profesa na Mkuu wa vitivo katika taasisi kadhaa za kitaalamu zenye hadhi ya juu, baada ya kuhadhiri na kufundisha kozi za dini, theolojia, falsafa, na mafunzo ya Biblia katika taasisi za elimu ya juu kama vile Chuo cha Wheaton, Chuo Kikuu cha St. Ambrose, Programu ya Shahada ya Uzamili ya Theolojia ya Chuo Kikuu cha Houston, Kitengo cha Dini cha Chuo Kikuu cha Iowa, na Taasisi ya Mafunzo ya Ibada ya Robert E. Webber. Ameandika idadi kubwa ya vitabu, mitaala, na nyenzo za kujifunzia ili kuwaandaa viongozi wa mijini, ikijumuisha mtaala wa mafunzo wa Capstone (hii ni programu mama ya TUMI yenye moduli 16 za hadhi ya mafunzo ya seminari, yanayotolewa kupitia mfumo wa elimu ya masafa), Mizizi Mitakatifu: Kidokezo cha Namna ya Kurejesha Mapokeo Makuu , ambayo inaangazia namna makanisa ya mijini yanavyoweza kufanywa upya kupitia kugundua upya imani halisi, sahihi ya kihistoria; na Mweusi na Mwanadamu: Kumgundua Upya M.L. King kama Nyenzo ya Theolojia na Maadili ya Weusi . Dkt. Davis pia ameshiriki katika mihadhara ya kitaalamu kama the Staley Lecture series, makongamano ya kufanywa upya kama Promise Keeper Rallies na miungano ya kithiologia kama The University of Virginia Lived Theology Project Series. Vilevile alipokea tuzo ya heshima ya mwanafunzi mashuhuri ( Alumni Fellow Award ) kutoka Chuo Kikuu cha Iowa cha Sanaa na Sayansi za Kiliberali mnamo 2009. Dkt. Davis pia ni mwanachama wa The Society of Biblical Literature, na The American Academy of Religion .
/ 5
K U T A F S I R I B I B L I A
Utangulizi wa Moduli
Salamu katika Jina lenye Nguvu la Yesu Kristo! Kulingana na ushahidi wa wazi wa maandiko yenyewe, Mungu huwaandaa wawakilishi wake kupitiaNeno laMungu lililovuviwa naRoho, yaaniMaandiko. Kila mtu ambaye Mungu anamwita katika huduma lazima adhamirie kujinidhamisha ili aweze kuwa mahiri katika Neno, kutii maagizo ya Neno, na kufundisha kweli ya Neno la Mungu. Kama mtenda kazi, lazima ajitahidi kutumia kwa halali Neno la kweli, na hivyo kukubaliwa na Bwana katika jitihada zake kujifunza (2 Tim. 2:15). Moduli hii inaangazia kweli, kanuni na athari za kufasiri Biblia. Katika somo letu la kwanza, Kuvuviwa kwa Biblia: Chimbuko na Mamlaka ya Biblia , tutaonyesha uhitaji wa kutafsiri Biblia na nini tunahitaji kufanya ili kujiandaa kwa kazi hii kubwa. Tutaangazia kwa kina pande zotembili zaBiblia, upandewa uungunawa kibinadamu, tutafafanua lengo la tafsiri zote, na kuweka wazi mawazo yetu ya kitheolojia kuhusu nafasi ya juu ya Maandiko katika Kanisa. Tutakazia hasa juu ya aina ya maisha na matayarisho ya moyo yanayohitajika ili kufasiri Neno la Mungu kwa usahihi. Pia tutaangalia madai ya Biblia kuwa imevuviwa na Mungu, na mamlaka na nafasi yake katika maazimio ya kitheolojia na kiroho katika Kanisa. Katika nyakati hizi ambazo kuna mlipuko mkubwa na kuenea kwa elimu ya Biblia, pia tutaangalia kwa ufupi uhakiki wa kisasa wa Biblia ( Biblical criticism ), na kuchunguza madai yake kama yanavyohusiana na kujifunza kwetu Maandiko katika nyakati hizi. Katika somo letu la pili, Hemenetiki ya Biblia: Mbinu ya Hatua Tatu, tutaonyesha njia bora zaidi ya kutafsiri Biblia iliyotengenezwa ili kukusaidia katika kujifunza Maandiko ili kuziba pengo liliopo kati ya ulimwengu ule wa zamani na huu wa sasa. Tunaiita Mbinu ya Hatua Tatu: fahamu hadhira asilia, gundua taratibu na kanuni kwa ujumla wake, na kisha uhusianishe utendaji katika maisha ya mtu. Katika somo hili, pia tutachunguza kifungu cha Maandiko kinachotumia mbinu hii, tukiangalia kifungu katika nyaraka za Paulo kwaWakorintho, katika waraka wake wa kwanza, 9:1 14. Kwa kutumia mfumo unaopatikana katika kiambatanisho chako cha Funguo za Ufafanuzi wa Biblia, tutachunguza kifungu hiki muhimu cha Maandiko tukiangalia hasa jinsi njia ya udhati, umakini na ya maombi inavyoweza kutuletea ujuzi na faraja kubwa tunapojitahidi kuyaelewa mapenzi ya Mungu kupitia Neno lake takatifu. Katika somo letu la tatu lenye kichwa Fasihi ya Kibiblia: Kutafsiri Tanzu za Biblia , tunaangazia aina za fasihi zinazopatikana katika Biblia na jinsi ya kuzifasiri. Tutafafanua na kubainisha dhana ya Tanzu katika ufasiri wa kibiblia, tukiweka muhtasari wa dhana hiyo, na kutoa mawazo machache ya msingi kuhusu aina hii ya hemenetiki maalum. Kisha tutajadili miundo mbalimbali za tanzu za kibiblia,
6 /
K U T A F S I R I B I B L I A
lakini tutajikita kuangazia kwa kina aina mbili za fasihi ambazo zinawakilisha sehemu kubwa ya Maandiko ya simulizi na ya kinabii katika Biblia. Tutajadili kwa ufupi lakini kwa kina juu ya elimu kwa njia ya simulizi (yaani, theolojia ya hadithi) pamoja na fasihi ya kinabii hasa ile ihusuyo mambo ya siku za mwisho, tukionyesha namba ambavyo kuzingatia matumizi ya tanzu kunaweza kutusaidia kufasiri Maandiko vyema zaidi. Hatimaye, tutahitimisha moduli yetu kwa somo la nne, Masomo ya Biblia: Kutumia Zana za Kujifunzia katika Kujifunza Biblia . Hapa tutachunguza aina za zana thabiti za kitaalamu tunazoweza kuzipata na kuzitumia kama rejea tunapojaribu kuelewa maana ya maandiko ya Biblia. Mwanafunzi wa Biblia leo anaweza kupata zana nyingi na nzuri, zilizoandikwa na kuhifadhiwa katika nakala mango na zinazopatikana mitandaoni; zote hizo zinaweza kumsaidia kupata umahiri katika Neno. Tutazingatia kwanza zana za msingi za ufasiri thabiti wa kibiblia: tafsiri nzuri ya Maandiko, visaidizi vya Kiebrania na Kiyunani, kamusi ya Biblia, konkodansi, na vitabu vya Mafafanuzi ya Maandiko ( exegetical commentaries ). Pia tutaangalia zana za ziada zinazoweza kuboresha na kuleta ufanisi katika kujifunza Maandiko. Hizo zitahusisha zana za rejea, Biblia za mada, Biblia zenye rejea, na konkodensi za mada. Pia tutazungumzia visaidizi vinavyowekea mkazo historia na desturi za Biblia: Kamusi za Biblia, ensaiklopidia ya Biblia, atlasi, na vitabu vingine vya rejea vya aina hiyo. Hatimaye, tutaangalia kwa ufupi vitabu vya mwongozo wa Biblia, Biblia za kujifunzia, na visaidizi vingine, na kuhitimisha somo letu kwa kuangaliza matumizi ya vitabu vya ufafanuzi wa Biblia, na kazi ya zana hizi kwa ujumla katika kutafsiri Biblia yako kwa ajili ya ibada, kuhubiri, na kufundisha. Hoja ya pekee ya Biblia yenyewe kwamba ina nguvu ya kubadilisha maisha inapaswa kuwa sababu ya kutosha kutupatia changamoto ya kulifahamu Neno la Mungu. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” 2 Tim. 3:16-17. Neno la Mungu lenye pumzi ya Mungu lililowasilishwa kupitia maneno ya wanadamu linatosha kututajirisha, kutufurahisha, na kutupa uwezo na ujuzi kwa ajili ya kila kazi njema. Kwa kweli, Neno la Mungu haliwezi kubatilishwa, sikuzote litatimiza kusudi lake, na litahakikisha mtu wa Mungu anafurahia mafanikio mema katika yote anayofanya ili kuendeleza Ufalme wa Mungu popote alipo ( Yoh. 10:35; Isa. 55:8-11; Yos. 1:8). Ombi langu la dhati ni kwamba baraka hizi zote na zaidi ziwe zako kadiri Roho Mtakatifu anavyokuwezesha kuzielewa kanuni na mbinu za kufasiri Neno lake takatifu na la milele! Ninayo matarajio makubwa ya kwamba utajengwa kupitia masomo haya. ~Mchungaji Dkt. Don l. Davis
/ 7
K U T A F S I R I B I B L I A
Mahitaji ya kozi
• Biblia (kwa madhumuni ya kozi hii, Biblia yako inapaswa kuwa tafsiri [mf. BHN, SUV, NEN, SRUV, au NIV, NASB, RSV, KJV, NKJV, ikiwa utatumia Biblia ya Kiingerezan.k.], na sio Biblia iliyofafanuliwa [mf. The Living Lible, The Message ]). • Kila moduli katika mtaala wa Capstone imeainisha vitabu ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza moduli husika. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya Capstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata orodha ya vitabu vinavyohitajika kwa ajili ya moduli hii. • Daftari na kalamu kwa ajili ya kuchukua maelezo na kufanyia kazi za darasani. • Douglas, J. D., N. Hillyer, and D. R. W. Wood, eds. New Bible Dictionary , 3rd ed. Downers Grove: Intervarsity Press (IVP), 2000. • Strong, james. Strong’s Exhaustive Concordance of the Bible . Iowa falls: World bible Publishers, 1986. • Vine, W. E. Vine’s Complete Expository Dictionary of Old and New Testament Words . Merrill F. Unger and william white, jr., revision eds. Nashville: Thomas nelson, 1996. • Wenham, G. J., J. A. Motyer, D. A. Carson, and R. T. France, eds. New Bible Commentary . 21st Century ed. Downers Grove: IVP, 2000. • Kuhatschek, Jack. Applying The Bible . Grand Rapids: Zondervan, 1990. • Montgomery, J. W. Ed. God’s Inerrant Word . Minneapolis: Bethany, 1974. • Packer, J. I. “Fundamentalism” And The Word Of God . London: IVP, 1958. • ------. God Has Spoken: Revelation And The Bible . Grand Rapids: Baker, 1979. • Sproul, R. C. Knowing Scripture . Downers Grove: IVP, 1977.
Vitabu na machapisho yanayohitajika
Vitabu vinavyopendekezwa kununuliwa. Tafadhali zingatia: unasisitizwa kununua nyenzo hizi kwa ajili ya maktaba yako binafsi. Utahitaji kuwa nazo kwa ajili ya kukamilisha kazi zinazotolewa.
Vitabu vya rejea
8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Muhtasari mfumo wa kutunuku matokeo na uzito wa gredi.
Matakwa ya kozi
Mahudhurio na ushiriki darasani . . . . . . . 30% Majaribio . . . . . . . . . . . . . . . . . 10% Mistari ya kukumbuka. . . . . . . . . . . . 15% Kazi za Ufafanuzi wa maandiko. . . . . . . . 15% Kazi za huduma. . . . . . . . . . . . . . 10% Usomaji na kazi za kufanya nyumbani. . . . . 10% Mtihani wa mwisho. . . . . . . . . . . . . 10%
alama 90 alama 30 alama 45 alama 45 alama 30 alama 30
alama 30 Jumla: 100% alama 300
Mambo ya kuzingatia katika utoaji maksi
Mahudhurio na ushiriki darasani
Kuhudhuria kila kipindi ni moja ya masharti ya msingi ya kozi hizi. Kukosa kipindi kutaathiri matokeo yako. Ikiwa una dhararua isiyoepukika itakayokulazimu kukosa kipindi, tafadhali mjulishe mkufunzi wako mapema. Ukikosa kipindi ni jukumu lako kutafuta taarifa kuhusu kazi na mazoezi uliyokosa, na kuongea na mkufunzi wako pale inapobidi kufanya na kukabidhi kazi na mazoezi kwa kuchelewa. Sehemu kubwa ya mafunzo yanayohusiana na kozi hii hufanyika kupitia mijadala. Kwa hivyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha darasa. Kila kipindi kitaanza na jaribio dogo kuhusu mawazo ya msingi yaliyofundishwa katika somo lililopita. Njia nzuri zaidi ya kujiandaa na majaribio haya ni kupitia Kitabu cha Mwanafunzi na daftari uliloandikia maelezo ya somo hilo lililopita. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa kutamka au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. Neno la Mungu ni zana yenye nguvu ambayo Mungu anaitumia ili kuwaandaa watumishi wake kwa kila kazi ya huduma aliyowaitia (2 Tim. 3:16-17). Ili kutimiza matakwa ya kozi hii, lazima uchague kifungu cha Biblia na kufanya uchambuzi wa kina (yaani, ufafanuzi wa Maandiko). Kazi yako iwe na kurasa tano ziliyochapwa kwa kuacha nafasi mbili kati ya mistari au kuandikwa vizuri kwa mkono. Uchambuzi wako ujikite katika mojawapo ya maeneo manne ya Neno la Mungu yaliyofundishwa katika masomo manne ya kozi hii. Ni shauku na matumaini yetu kwamba utashawishika kikamilifu na kuamini juu ya uwezo wa Maandiko kubadilisha na kuleta athari chanya katika maisha yako na ya wale
Majaribio
Kukariri mistari ya Biblia
Kazi za ufafanuzi wa Maandiko
/ 9
K U T A F S I R I B I B L I A
unaowahudumia. Unapoendelea kujifunza kozi hii, uwe huru kuongeza mistari kadhaa katika uchambuzi wako (mfano mistari 4-9) kuhusu jambo ambalo ungependa kujifunza kwa kina. Maelezo yote kuhusiana na kazi hii yametolewa katika ukurasa wa 10-11, na yatajadiliwa katika sehemu ya utangulizi ya kozi hii. Matarajio yetu ni kwamba wanafunzi wote watatumia mafunzo haya kivitendo katika maisha yao na katika majukumu yao ya kihuduma. Mwanafunzi atakuwa na jukumu la kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa kutumia kanuni alizojifunza katika mazingira halisi ya huduma. Maelezo ya namna ya kufanya mafunzo kwa vitendo yanapatika katika ukurasa wa 12, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi wa kozi. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu chako cha Mwanafunzi. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Jedwali la Tathimini ya Usomaji” lililomo katika Kitabu cha Mwanafunzi, kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. Mwisho wa kozi, Mkufunzi wako atakupa mtihani wa mwisho utakaofanyia nyumbani. Katika mtihani huu hutaruhusiwa kutumia vitabu vyako vya kozi hii isipokuwa Biblia. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya yale uliyojifunza katika kozi na namna yanavyoathiri mfumo wako wa fikra na utendaji wako katika huduma. Utakapokabidhiwa mtihani wa mwisho, mkufunzi wako atakupa taarifa zaidi kuhusu tarehe za kukamilisha na kukabidhi mtihani wako na kazi nyinginezo.
Kazi za huduma
Kazi za darasani na za nyumbani
Usomaji
Mtihani wa mwisho wa kufanyia nyumbani
Gredi za ufaulu
Mwishoni mwa kozi hii, gredi zifuatazo zitatolewa na kuhifadhiwa kwenye mbukumbu za kila mwanafunzi. A – Bora D – Inaridhisha B – Nzuri sana F – Hairidhishi (Feli) C – Nzuri I – Isiyokamilika
1 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa kutumia mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi zako za ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako, hivyo ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika kusoma moduli hii ya Kutafsiri Bibliaya mtaala wa Capstone , utahitajika kufanya kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (kujifunza kutokana na Maandiko yenyewe) kwa kutumia andiko mojawapo kati ya Maandiko yafuatayo ya Neno la Mungu: Zaburi 19:7-11 2 Timotheo 3:14-17 1 Wakorintho 2:9-16 Zaburi 1:1-3 Mathayo 22:34-40 Yakobo 1:22-25 Isaya 55:8-11 2 Petro 1:19-21 Mithali 2:1-5 Dhumuni la kazi hii ya ufafanuzi ni kukupa fursa ya kujifunza kwa kina andiko mojawapo muhimu linalozungumzia asili na kazi ya Neno la Mungu. Unaposoma mojawapo ya maandiko yaliyopo hapo juu (au andiko ambalo wewe na Mkufunzi wako mtakubaliana ambalo linaweza kuwa halipo kwenye orodha hii), matumaini yetu ni kwamba utaweza kuonyesha jinsi andiko hilo linavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu katika kuimarisha maisha yetu ya kiroho na kwa faida ya maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia ni maombi yetu kwamba Roho akupe ufahamu wa jinsi unavyoweza kuhusianisha moja kwa moja maana ya andiko hilo na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya ufafanuzi, ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika ? Kazi za Ufafanuzi wa Maandiko
Dhumuni
Muhtasari na Muundo
/ 1 1
K U T A F S I R I B I B L I A
2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa pamoja na sisi leo ? 3. Ni kitu gani Roho Mtakatifu ananiagiza kufanya kupitia kanuni hii, leo, katika maisha na huduma yangu ? Baada ya kuwa umeyajibu maswali haya katika kujifunza kwako kibinafsi, hapo sasa utakuwa tayari kuendelea kuandika ulichokigundua katika kazi uliyopewa . Angali hapa chini mfano wa muhtasari wa kazi yako: 1. Eleza kile unachoamini kuwa ndio mada kuu au wazo kuu la andiko ulilochagua. 2. Eleza kwa muhtasari maana ya andiko hilo (unaweza kufanya hivi katika aya mbili au tatu, au, ukipenda, kwa kuandika ufafanuzi mfupi wa mstari kwa mstari juu ya kifungu husika). 3. Eleza kanuni kuu moja hadi tatu au maarifa ambayo kifungu hiki kinatoa kuhusu Neno la Mungu. 4. Eleza jinsi kanuni moja, kadhaa, au zote zinaweza kuhusiana na yafuatayo: Kwa msaada au mwongozo, tafadhali uwe huru kusoma vitabu vya rejea vya kozi hii na/au vitabu vya ufafanuzi ( commentaries ), na kutumia maarifa yaliyomo katika vyanzo hivyo katika kazi yako. Unapotumia maarifa au mawazo ya mtu mwingine kujenga hoja zako, hakikisha unatambua kazi za waandishi husika kwa kutaja vyanzo vya taarifa hizo. Astahiliye heshima apewe heshima yake. Tumia marejeleo ya ndani ya maandishi ( in-text-refences ), tanbihi ( footnotes ), au maelezo ya mwisho ( endnotes ). Njia yoyote utakayochagua kutaja rejea zako itakubalika, ilimradi 1) utumie njia hiyo moja katika kazi nzima, na 2) uonyeshe pale unatumia mawazo ya mtu mwingine, na umtambue mwandishi husika kwa kumtaja. (Kwa maelezo zaidi, angalia katika Kiambatisho cha Jinsi ya Kuandika Kazi Yako: Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua Waandishi wa Vitabu vya Rejea .) Kabla hujakabidhi kazi yako, hakikisha inasifa zifuatazo: • Imeandikwa au kuchapwa vizuri na inasomeka na kueleweka. a. Kiroho chako binafsi na namna unavyotembea na Kristo b. Maisha na huduma yako katika kanisa lako la mahali pamoja c. Hali au changamoto katika jamii yako kwa ujumla.
• Ni uchambuzi wa mojawapo ya vifungu hapo juu. • Imekusanywa kwa wakati (haijacheleweshwa).
1 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
• Ina urefu wa kurasa 5. • Inafuata muhtasari au mpangilio uliotolewa hapo juu, na imeandikwa kwa namna ambayo msomaji ataweza kuelewa. • Inaonyesha jinsi kifungu husika kinavyohusiana na maisha na huduma leo. Usiruhusumaagizo haya yakuogopeshe; hii ni kazi ya kujifunza Biblia! Unachohitaji kuonyesha katika kazi hii ni kwamba ulisoma andiko husika, umeeleza kwa muhtasari maana yake, ukaweza kupata kanuni chache muhimu kutoka katika andiko hilo, na kuzihusianisha na maisha na huduma yako mwenyewe. Kazi ya ufafanuzi inabeba alama 45 na inawakilisha 15% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi yako kuwa bora na yenye maarifa ya kutosha ya Neno la Mungu. Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo (Waebrania 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, sio wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa na sisi kujitazama sura zetu za asili kwenye kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila afanyacho (Yakobo 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa sababu hiyo, kama takwa mojawapo muhimu la kukamilisha moduli hii, utatakiwa kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo ambapo utaweza kuwashirikisha wengine sehemu ya maarifa ambayo umejifunza katika kozi hii. Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kutimiza takwa hili la kujifunza kwako. Unaweza kuchagua kuwa na muda wa kujifunza na mtu binafsi, kutumia madarasa ya shule ya uanafunzi, vikundi vya vijana au watu wazima, au hata kwa kupata nafasi ya kuhudumu mahali fulani. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajadili na hadhira baadhi ya maarifa uliyojifunza kutoka darasani. (bila shaka, unaweza kuchagua kushirikiana nao baadhi ya maarifa toka katika kazi yako ya Ufafanuzi wa Maandiko ya moduli hii). Kazi ya huduma
Utoaji maksi
Dhumuni
Mpangilio na Muhtasari
/ 1 3
K U T A F S I R I B I B L I A
Uwe huru na tayari kubadilika na kuendana na mazingira yoyote unapofanya kazi yako. Ifanye iwe yenye ubunifu na inayoruhusu kusikiliza mitazamo tofauti kwa nia ya kujifunza. Fanya uchaguzi mapema kabisa kuhusu aina ya muktadha ambao unatamani kutumia kushirikisha watu wengine maarifa haya na kisha mshirikishe Mkufunzi wako juu ya maamuzi hayo. Panga hayo yote mapema na epuka kusubiri dakika za mwisho kuamua na kutekeleza kile unachotaka katika kazi yako. Baada ya kutekeleza kazi yako, andika kwa ufupi (ukurasa mmoja) tathmini ya kazi yako na umkabidhi mkufunzi wako. Mfano wa muhtasari wa Kazi ya Huduma ni kama ifuatavyo: 1. Jina lako 2. Eneo ulilolitumia na hadhira uliyowashirikisha. 3. Muhtasari kidogo namna muda ulivyoenda, namna ulivyojisikia na namna watu walivyoitikia. 4. Ulijifunza nini kupitia mchakato mzima wa kazi yako. Kazi ya huduma inabeba alama 30 ambazo zinawakilisha 10% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha unashirikisha yale uliyojifunza kwa ujarisi na ripoti yako iwe yenye kueleweka vizuri.
Utoaji maksi
/ 1 5
K U T A F S I R I B I B L I A
Kuvuviwa kwa Biblia Chimbuko na Mamlaka ya Biblia
S O M O L A 1
page 309 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kufafanua hemenetiki kama taaluma na tawi la maarifa linalohusika na ufasiri, hasa ufasiri wa maandiko. • Kutoa ushahidi kwamba Biblia lazima itafsiriwe kama kitabu cha kimungu na cha kibinadamu, chenye viwango vyote viwili ili kufahamu na kuelewa kikamilifu asili ya maandiko. • Kuonyesha mambo ya msingi ambayo Wakristo katika historia wameamini kuhusu asili ya maandiko ikijumuisha asili ya kiroho ya maandiko, andiko kutafsiri andiko, dhana ya ufunuo endelevu, Kristo kama kiini cha maandiko, na umuhimu wa Roho Mtakatifu ili kulielewa Neno la Mungu. • Kutoa muhtasari wa Mbinu ya Hatua Tatu ya Kutafsiri Biblia inayohusisha kuelewa muktadha asilia wa andiko, kugundua kanuni za Biblia katika andiko, na kuhusianisha maana ya andiko husika na maisha yetu. • Kuainisha hatua mbalimbali zinazohusika katika kuuandaa moyo kwa ajili ya kazi ya kutafsiri Biblia, ikijumuisha hitaji la unyenyekevu na maombi, bidii na kudhamiria, na kujishughulisha kwa bidii na Biblia kama mtendakazi. • Kuonyesha ufahamu wako juu ya aina za majukumu tunayopaswa kuchukua tunapotayarisha akili zetukwa ajili kazi yakutaifsiri Bibliakwakina, ikijumuisha jukumu la mtafiti, jukumu la mpelelezi, na jukumu la mwanasayansi— kuchunguza Neno kwa bidii, kufuatilia kwa ukaribu mawazo mbali mbali, na kupima kila ushahidi kwa umakini kabla ya kutoa hukumu. • Kutumia maandiko yenyewe kuthibitishasha madai yake kwamba Biblia imevuviwa na Roho wa Mungu na vilevile ya kwamba imeandikwa na waandishi wa kibinadamu. • Kuonyesha na kutofautisha kati ya nadharia mbalimbali za uvuvio ambazo zinajaribu kuelezea ni jinsi gani na kwa namna gani maandiko yanaweza kuthibitishwa kuvuviwa na Roho Mtakatifu na wakati huo yakatokana na kazi ya uandishi wa kibinadamu.
Malengo ya somo
page 311 2
1
1 6 /
K U T A F S I R I B I B L I A
• Kuonyesha kwa uangalifu mantiki na historia ya uhakiki wa Biblia, na jinsi taaluma hii ya kisasa inavyotafuta kufuatilia asili ya maandiko kwa kuanzia na matukio ya awali yanayonenwa katika Biblia hadi simulizi halisi za matukio hayo yaliyorekodiwa katika vitabu vya kikanoni vya maandiko. • Kutoa maelezo mafupi yanayojumuisha faida na changamoto zinazohusiana na vipengele vikuu vya uhakiki wa kisasa wa Biblia, kama muundo, chanzo, kiisimu, kimaandishi, kifasihi, kikanoni, uhakiki wa kiuchunguzi, na uhakiki wa kihistoria, pamoja na utafiti juu ya tafsiri. Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; 7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. 8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. 9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. 10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; 11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. ~ Isaya 55:6-11 Mungu hana mashaka kabisa katika madai yake ya uaminifu na ukweli mkamilifu. Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ni Mungu wa uaminifu na kuaminiwa, ambaye hajawahi na hawezi kamwe kusema uongo au kujuta, ambaye Neno lake ni kweli, na ambayemamlaka na kweli yake huwapa watu wake ujasiri katika yeye. Hata ukitazama baadhi ya maandiko ya Biblia kuhusu uaminifu wa Mungu yanasisitiza kwa uhakika wa kiwango cha juu kwamba Mungu ni Mungu mwaminifu katika Neno la Agano lake, na ametamka kwa ujasiri kuhusu nguvu ya Neno lake na ahadi zake. Yafuatayo ni machache tu kati ya maandiko yanayoonyesha ujasiri na uhakika wa Neno la Mungu. Zaburi 19:7-10 – Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima. 8 Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru. 9 Kicho cha Bwana ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za Bwana ni kweli, Zina haki kabisa. 10 Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali. Msingi wa ujasiri wetu
1
Ibada
page 312 3
/ 1 7
K U T A F S I R I B I B L I A
Kumbukumbu la Torati 32:4 – Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili . Kutoka 34:6 – Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli . Zaburi 98:3 – Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Zaburi 100:5 – Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi. Isaya 25:1 – Ee Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli. Yohana 6:63 – Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. 1 Petro 1:23-25 – Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. 23 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. Ukiongeza kwenye orodha hii ndogo maandiko mengi yaliyopo kuhusu uaminifu wa Mungu, kwa hakika yatakuleta kwenye hoja za msingi za Isaya 55. Mungu analinganisha uhakika wa utimilifu wa Neno lake, kwa maana ya unabii na ahadi zake, na nguvu ya kikaboni ya mvua kutoka mbinguni, ambayo ikishachanganyika na mbegu na ardhi, huzaa matunda mengi. Kimsingi Mungu anamaanisha kwamba Neno lake lina matokeo, ni hakika, linafanikiwa, na lina nguvu kama vile mvua inavyochanganyika na chembe za ardhi. Ni kitu gani kinachotupa uhakika huu wa matokeo? Ahadi hii kwamba Neno la Mungu litaleta matokeo na ustawi inamsingi gani? Uhakika huu umejikita katika tabia yake, ndani ya nafsi yake, katika ukweli wake kama Mungu mwaminifu, Mungu asiyeweza kusema uongo (Tito 1:2), ambaye Neno lake ni kweli na hakika, limethibitishwa milele mbinguni. Daudi aliimba kuhusu uaminifu wa Mungu na kutegemeka kwa Neno lake katika Zaburi 89: “Fadhili za Bwana nitaziimba milele; Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako. 2 Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele; Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.” (Zab. 89:1-2). Katika andiko hili Mungu anatuhakikishia kwamba Neno lake ni kweli. Kwa sababu yeye ni Mungu mwaminifu, Neno lake litatimiza yale ambayo Mungu ameyakusudia na kufanikiwa katika kila jambo, na kila jukumu na kazi ambayo ameliagiza kufanya.
1
1 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Hebu nikuulize: unaamini nini ni msingi wa ujasiri na imani yetu ya kwamba yote ambayo Mungu ametuahidi yatatimia—ni kwa misingi gani na kwa ushahidi gani tunaamini kwamba tutapokea uzima tulioahidiwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo? Jibu ni tabia na asili ya Mungu Aliye Hai ya ukweli na unyoofu, yeye ambaye daima amesema yaliyo kweli kwa watu wake. Mungu wetu ni Mungu wa kweli, na kwa sababu hiyo tunashikilia ahadi za Mungu, tukijua yakini kwamba kile alichoahidi atafanya. Huu ndio msingi pekee wa ujasiri wetu. Baada ya kutamka na/au kuimba Imani ya Nikea (iliyo katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Bwana mbarikiwa, uliyefanya Maandiko Matakatifu yote yaandikwe ili kutufundisha: Utujalie tuyasikie, tuyasome, tuyatie alama, tujifunze na kuyatafakari kwa undani, ili tupate kulikumbatia na kulishikilia daima tumaini lenye baraka la uzima wa milele, ambalo umetupa katika Mwokozi wetu Yesu Kristo; anayeishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele. Amina. ~ Episcopal Church. The Book of Common Prayer and Administrations Of The Sacraments And Other Rites And Ceremonies Of The Church, Together With The Psalter Or Psalms of David . New York: The Church Hymnal Corporation, 1979. uk. 236
Kanuni ya Imani ya Nikea na maombi
1
Hakuna Jaribio katika somo hili.
Jaribio
Hakuna maandiko ya kukariri katika somo hili
Mazoezi ya kukariri maandiko
Hakuna kazi katika somo hili
Kazi za kukusanya
/ 1 9
K U T A F S I R I B I B L I A
MIFANO YA REJEA
Kwa Nini Tunapaswa Kujali?
Watu wengi nyakati za leo wanaamini kirahisi tu kwamba sayansi imefanikiwa kushusha thamani ya Biblia kama kitabu cha kuaminika, angalau kwa maana ya ushahidi wa madai ya kihistoria na uwezekano wa uwepo wa nguvu zisizo za kawaida [yaani nguvu za kiungu]. Kikundi fulani kidogo lakini chenye sauti cha wanafunzi watiifu wa Biblia kinaamini kuwa ni wajibu wao kuwathibitishia wale wanaotilia shaka asili ya Biblia kwamba Biblia ina usahihi na ukweli wa kihistori. Kama msingi wa hoja zao, wanataja kutimia kwa unabii, usahihi wa utabiri uliomo katika Biblia, muunganiko wa ndani wa ujumbe wa Biblia, na namna Biblia ilivyohifadhiwa kama uthibitisho wa kwamba Biblia yetu imevuviwa na Mungu. Wakati huo kundi jingine la Wakristo waaminifu na watiifu vilevile, japokuwa hawana sauti ukilinganisha la kwanza, linaamini kwamba huwezi kutumia ushahidi wa namna hiyo kuwashawishi wale wasioiamini Biblia juu ya uhalali wake wa kihistoria na kiroho. Wao wanaamini kwamba bila Roho Mtakatifu hakuna mtu atakayeweza kushawishiwa na madai na ahadi za Mungu katika Kristo. Kwa msingi huo, hata kushindana kwetu kwa hoja za kawaida na wakosoaji wa Biblia hakutaweza kuwafanya waiamini. Unapozingatia misimamo hii, kwa nini unaamini kwamba tunapaswa kutilia maanani au kutojali kuhusu hoja ya asili ya Biblia, mamlaka yake, na uvuvio wa Mungu? Wakristo wa Kiinjili wameandika maelfu ya vitabu juu ya umuhimu wa kutumia njia na kanuni bora katika kuielewa Biblia. Mtu anaweza kwenda kwenye duka lolote la vitabu la Kikristo au maktaba ya seminari na kupata nyenzo nyingi zote zikitoa maelekezo ya kina kuhusu hatua mahususi tunazopaswa kuchukua ili kugundua “maana iliyo wazi na ya moja kwa moja” ya maandiko ya Biblia. Pamoja na uwepo wa vitabu hivi vyote, bado tuna makanisa mengi ambayo yanadhihirisha ukosefu mkubwa wa ujuzi wa Biblia, na, licha ya kupata mbinu nzuri za jinsi ya kuendesha mafunzo ya Biblia, hawaonekani kupenda au kusoma Biblia zao zaidi kuliko wengine. Wengine wanadai kwamba utitiri wa mbinu hausaidii chochote pasipo uongozi na ujazo wa Roho Mtakatifu. Hawa wanaweza kufikia hatua ya kubeza na kudharau mbinu kabisa, na kusisitiza vigezo vya kiroho vya kutafsiri Biblia badala ya vigezo vya kiakili. Kwa vile Roho ndiye aliyeivuvia Biblia, ni lazima yeye pia aweze kuiangazia ili ieleweke. Je, kuna uhusiano gani kati ya mbinu na kazi ya Roho katika ufasiri wa kibiblia? Je, kuna njia nyingine yoyote inayoweza kutusaidi kuielewa Biblia kwa kiwango cha kubalisha maisha, nje ya kuangaziwa na Roho Mtakatifu, hata kama tunazo aina bora za hemeniti? Maandiko na Roho Mtakatifu
1
page 313 4
1
2
2 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Ni Fasihi au ni Neno Hai la Mungu, au Vyote viwili?
Kwa miongo michache iliyopita wasomi wachache wamekazia umuhimu wa kuielewa Biblia kama fasihi ili kugundua kile inachotufundisha kuhusu maisha yetu. Wanasema kwamba fasihi hufanya kazi kulingana na kanuni na mifumo iliyofafanuliwa, iwe ya kibiblia au la. Badala ya kuisoma Biblia kama kitabu cha kibinadamu chenye miundo na kanuni za kibinadamu, wasomi hao wanadai kwamba tumeikata Biblia katika vipande vidogovidogo, tukapuuza miundo ya fasihi, na kujaribu kutumia Biblia hasa kama nyenzo ya ushahidi katika kuthibitisha madai ya kitheolojia kuhusu hili, lile, au mada ile nyingine. Wengine wanadai kwamba ingawa Biblia iliandikwa na waandishi wa kibinadamu, maandishi hayo ni zaidi ya miundo tu na kanuni za kifasihi. Ni Neno la Mungu lililo hai, na tunapaswa kugundua na kuchota ndani yake (na, kwa hakika, kila mahali ndani yake) maana na ufahamu kuhusu wokovu na imani yetu katika Yesu Kristo. Je, nini mtazamo wako juu ya mjadala huu: je, Biblia ni kitabu cha fasihi, Neno la Mungu lililo hai, au vyote viwili?
3
1
Kuvuviwa kwa Biblia: Chimbuko na Mamlaka ya Biblia Sehemu ya 1: Kujiandaa kwa shughuli thabiti ya kutafsiri Biblia
YALIYOMO
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Hemenetiki ni taaluma na tawi la maarifa linalohusika na ufasiri, hasa ufasiri wa maandiko. Kama mbinu, hemenetiki inalenga kuelewa namna ambayo Biblia inapaswa kufasiriwa kama kitabu cha kimungu (cha kiroho) na cha kibinadamu, huku tukizingatia kwamba namna zote mbili za kuitazama Biblia (kiroho na kibinadamu) ni za muhimu ili kufahamu na kuelewa kikamilifu asili ya maandiko. Kihistoria Wakristo wenye kushika imani, tangu mwanzo, wameamini katika uvuvio wa maandiko, umuhimu wa andiko kufasiri andiko, na dhana ya ufunuo endelevu ambao unafikia kilele katika ufunuo wa Kristo. Ni kwa njia ya Roho Mtakatifu pekee maandiko yanaweza kueleweka. Mbinu ya Hatua Tatu ya ufasiri wa kibiblia inahusisha kuelewa muktadha asilia wa andiko, kugundua kanuni za kibiblia ndani ya andiko, na kuhusianisha maana ya andiko na maisha yetu. Ili kutafsiri Neno la Mungu kwa namna ifaayo, ni lazima tuandae mioyo yetu, akili zetu, na nia zetu kulisoma kwa unyenyekevu na kwa uthabiti, kulichanganua kwa uangalifu, na kulitii kwa moyo wote, yote haya kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Muhtasari wa Sehemu ya 1
/ 2 1
K U T A F S I R I B I B L I A
Lengo letu katika sehemu hii, Kujiandaa kwa shughuli thabiti ya kutafsiri Biblia, ni kukuwezesha kufahamu kwamba: • Hemenetiki ni taaluma na tawi la maarifa linahusika na ufasiri, hasa ufasiri wa maandiko. Hemenetiki ya Biblia inajikita hasa katika mbinu na sayansi ya kufasiri Biblia. • Kwa namna yoyote ile Biblia lazima ifasiriwe kama kitabu cha kimungu (cha kiroho) na cha kibinadamu, huku tukizingatia kwamba namna zote mbili za kuitazama Biblia (kiroho na kibinadamu) ni za muhimu ili kufahamu na kuelewa kikamilifu asili ya maandiko. • Tangu mwanzo, imani ya Kikristo ya kweli imezingatia dhana fulani za msingi kuhusu asili ya maandiko, ikijumuisha asili yake ya kimungu, ulazima wa andiko kufasiri andiko, dhana ya ufunuo endelevu ambao unafikia kilele katika ufunuo wa Mungu katika nafsi ya Kristo, na ulazima wa utendaji wa Roho Mtakatifu ili kuelewa Neno la Mungu. • Mbinu ya Hatua Tatu ya ufasiri wa Biblia, inayolenga kuchukulia kwa uzito tofauti ya kihistoria na kiisimu (kisarufi) kati ya ulimwengu wa nyakati za Biblia na ulimwengu wetu wa sasa, inahusisha jitihada za kuelewa ujumbe kwa kuzingatia muktadha wake wa asili, kugundua kanuni za Biblia kutoka katika andiko husika, na hatimaye kuhusianisha maana ya andiko na maisha yetu. • Ili kulitafsiri kwa usahihi Neno la Mungu, ni lazima tuandae mioyo yetu, akili zetu, na nia zetu kulisoma kwa unyenyekevu na kwa uthabiti, kulichanganua kwa uangalifu, na kulitii kwa moyo wote, yote haya kwa ajili ya utukufu wa Mungu. • Tunaandaa mioyo yetu kwa njia ya kunyenyekea na maombi, bidii na kudhamiria, na kujishughulisha kwa bidii katika Neno la Mungu kama mtendakazi. Tunaandaa akili zetu kwa kuchukua majukumu ya mpelelezi, mtafiti, na mwanasayansi – kuchunguza Neno kwa bidii, kufuatilia kwa ukaribu mawazo mbali mbali, na kupima kila ushahidi kwa umakini kabla ya kutoa hukumu. Tunaandaa nia zetu kwa kulitii Neno, si kulisikia tu; na kwa kukumbatia ukweli kwamba hekima inatokana na kuitikia Neno la Mungu, si kulitafakari tu.
1
2 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
I. Uhitaji wa kuitafsiri Biblia
Muhtasari wa Video ya Sehemu ya 1
A. Misamiati iliyomo
1. “Hemenetiki” – taaluma na tawi la maarifa ambalo huzingatia tafsiri, hususani tafsiri ya matini.
2. “Kutafsiri” – kitendo au mchakato wa kutafsiri au kufafanua; kutoa maana na mantiki ya ujumbe, maandishi, au kitu fulani.
1
B. Kwa nini ni muhimu Biblia itafsiriwe
1. Biblia ni kitabu cha kimungu : hakuna ajuaye mawazo ya Mungu ila Mungu mwenyewe, 1 Kor. 2:10-11.
a. Mungu amesema wazi, Kumb. 30:11-14.
b. Mungu amesema ili kwamba mtafutaji apate kuelewa mawazo yake, Isa. 45:19.
c. Mungu amesema kwa ukamilifu (yaani, kutupa mambo ambayo tunahitaji kujua ili kumwamini na kumtii), Kumb. 29:29.
2. Biblia ni kitabu cha kibinadamu , 2 Pet. 3:15-16.
a. Kuna tofauti katika lugha, utamaduni na uzoefu.
/ 2 3
K U T A F S I R I B I B L I A
b. Maandiko yaliandikwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 1,600 na waandishi 40 tofauti, ambao uzoefu na uelewa wao ulikuwa tofauti kabisa na wetu.
3. Mungu anatuagiza tuyatumie maandiko kwa usahihi, yaani, tuyasome kwa namna ya kupata maana anayokusudia tuipate.
a. 2 Timotheo 2:15
1
b. 1 Wakorintho 2:6
c. 2 Wakorintho 4:2
C. Lengo la kutafsiri Biblia: kufanya maana iwe wazi na ya kueleweka
1. “Kutumia kwa halali” Neno la kweli, 2 Tim. 2:15
2. Kutoa maana na kuiweka wazi, Neh. 8:1-3, 7-8
3. Kuijua kweli na kupata uhuru wa Mungu, Yohana 8:31-32
4. Kunufaika kiroho kutokana na juhudi zetu katika Neno la Mungu, Zab. 19:7-11.
2 4 /
K U T A F S I R I B I B L I A
D. Mawazo muhimu ( mambo tutakayo kubaliana nayo kama kweli kabla ya kuanza kutafsiri maandiko )
1. Maandiko ni zao la uandishi wa kimungu na wa kibinadamu.
2. Ufasiri wa Kibiblia unahusu eksejesi a ( exegesis – ufafanuzi, uchambuzi), sio eisejesia ( eisegesis ).
1
a. Ufafanuzi – kueleza, kuweka wazi, na kufasiri maana kutoka ndani ya andiko (kutoa nje).
b. Eisejesia ( eisegesis ) – kuelezea na kufasiri matini, haswa maandiko ya kibiblia, kwa kutumia maoni yako mwenyewe ( yaani, kuingiza mawazo binafsi katika andiko ).
3. Ni lazima andiko litafsiri andiko.
a. 1 Wakorintho 2:13
b. Mathayo 22:29
c. Luka 24:44-47
4. Ufunuo endelevu : Ufunuo unafunuliwa hadi kufikia kilele kwa Yesu Kristo (yaani, Yesu ndiye kipimo ambacho kwacho tafsiri zote za maandiko zinapimwa na kuhakikiwa).
a. Waebrania 1:1-2
/ 2 5
K U T A F S I R I B I B L I A
b. Matayo 17:5
c. Yohana 1:17-18
d. 2 Wakorintho 4:3-6
5. Maandiko lazima yasomwe kwa kuangaziwa (kutiwa nuru) na Roho Mtakatifu.
1
a. 2 Petro 1:20-21
b. Marko 12:36
c. Matendo 1:16
d. Matendo 3:18
E. Muhtasari wa “Mbinu ya Hatua Tatu” ya kutafsiri Biblia
1. Elewa muktadha na hali ya asili: andiko haliwezi kumaanisha kile ambacho halijawahi kumaanisha.
2. Tafuta kanuni za jumla: Roho hufunua kweli za ulimwengu mzima katika Neno la Mungu, ambazo zina nguvu juu ya akili, dhamiri, na nia .
3. Husianisha maana ya andiko na maisha: Neno la Mungu linapaswa kuaminiwa na kutiiwa, si tu kuchambuliwa na kujifunza.
2 6 /
K U T A F S I R I B I B L I A
II. Hitaji la maandalizi ya moyo katika kutafsiri Biblia: Kuwa na moyo wa unyenyekevu. 2 Nyakati. 16:9a - Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake.
A. Tunalikaribia Neno la Mungu kwa unyenyekevu katika maombi: umuhimu wa maombi, Zab. 119:18.
1
1. Ombea uongozi wa Roho wa Mungu, 1 Yohana 2:20-21.
2. Omba uwazi wa maagizo ya Mungu, Zab. 32:8-9.
3. Ombea nguvu za Mungu za kukuwezesha kuamini na kutii.
a. Waebrania 11:6
b. Yakobo 1:22-25
4. Omba kwa ajili ya uongozi wa Mungu katika kuwashirikisha wengine, Ezra 7:10.
B. Mitazamo ya kuwa nayo katika kujifunza maandiko
1. Uwe mtenda kazi, mwenye bidii na dhamira ya dhati, Mit. 2:1-9; ling. Mit. 2:2-5; 2 Tim. 2:15.
2. Uwe mnyenyekevu na mwenye moyo uliopondeka, Isa. 57:15.
/ 2 7
K U T A F S I R I B I B L I A
3. Uwe mwenye kufundishika na moyo wa utayari, Zab. 25:4-5.
C. “Lima ardhi hiyo”: lifahamu Neno la Mungu kwa kulisoma na kulitafakari mara kwa mara na kwa bidii, Hos. 10:12.
1. Soma Biblia, Neh. 8:8.
2. Kariri Biblia, Zab. 119:11.
1
3. Tafakari Biblia, Zab. 1:1-3.
4. Sikiliza Biblia inapohubiriwa na kufundishwa (Matendo 17:11).
III. Hitaji la maandalizi ya akili katika kutafsiri Biblia: Kuwa mwenye akili thabiti 1 Wakorintho 14:20 – Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima.
A. Liendee Neno la Mungu kama mchunguzi (mtafutaji aliyedhamiria kugundua hazina yake), Mathayo 13:52.
1. Tambua kwamba ulimwengu wa Biblia ni tofauti kabisa na wakati huo huo unafanana sana na ulimwengu wetu.
2. Hatua ya kwanza ya kujifunza Biblia ni kuufahamu “ulimwengu wao”.
2 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
3. Kujifunza Biblia kwa namna yoyote kunahusisha “kusafiri katika wakati” kwa namna fulani.
4. Funguamacho yangu nipate kuona: kutazama, kushiriki, na kugundua.
B. Liendee Neno la Mungu kama mpelelezi (kutafuta vidokezo ili kuelewa maana pana na muunganiko wa ujumbe).
1
1. Nguvu ya ukweli imo katika yodi na nukta; umuhimu wa kujizoeza kutafuta vidokezo, Mt. 5:17-18.
2. Tafuta kwa ukamilifu kiasi cha kutopitwa na wazo hata moja: Agassiz na unaona nini? , Luka 16:16-17.
3. Fuatilia kila wazo kwa kadri iwezekanavyo; hoji kila shahidi wa maandiko.
4. Fuatilia kila kisa na ushahidi wake (mistari ya rejea).
5. Neno la Mungu haliwezi kupita (Luka 21:33).
C. Liendee Neno la Mungu kama mwanasayansi (aliyejitolea kuchunguza mawazo yote na kuthibitisha kila kitu kulingana na kweli), Mdo. 17:11.
1. Pima kila nadharia na dhana dhidi ya Neno, huku ukiyafanya mawazo yote kuwajibika kwa Neno la Mungu.
a. 1 Yohana 4:1
/ 2 9
K U T A F S I R I B I B L I A
b. Isaya 34:16
c. 1 Wathesalonike 5:21
d. Isaya 8:20
e. Warumi 12:2
1
f. Waefeso 5:10
g. Wafilipi 1:10
2. Usikubali maelezo yoyote ambayo hayana msingi katika Neno la Mungu.
a. 1 Yohana 4:5-6
b. 1 Petro 1:10-12
3. Jitahidi kuhusianisha maana ya kila andiko na Masihi.
a. 2 Timotheo 3:15-16
b. Yohana 5:39
3 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
4. Katika kufikiri kwako, fikiria kama mtu aliyekomaa.
a. Sahihisha ukweli wako; usitoe hukumu za haraka haraka au kutoa misimano juu ya mambo kwa taarifa za juu juu, Yoh. 7:24.
b. Tengeneza hoja zenye maana: mantiki na kanuni za kujenga dhana. (1) Kanuni ya utambulisho (“A ni A”) (2) Kanuni ya kutokupingana (“A sio B”) (3) Kanuni ya kati “ama, au” (“X ni ama A au B” – si A na B) c. Jifunze kufikiri kisuluhishi: A na B zote ni kweli (AB). (1) Kweli ya Mungu ni A: Yesu ni Mungu kamili (2) Kweli ya Mungu ni B: Yesu ni mwanadamu kamili (3) Kweli ya Mungu ni zote A na B (usawa, utofauti, umoja)
1
D. “Usizitegemee akili zako mwenyewe,” Mit. 3:5-6.
1. Jifunze kuahirisha hukumu yako hadi upate ukweli wote.
2. Jiwekee nidhamu ili kutokurupuka kufikia hitimisho.
3. Hakiki kila kitu ambacho unafikiri umekigundua.
4. Waruhusu wengine wahukumu matokeo ya uchunguzi wako.
/ 3 1
K U T A F S I R I B I B L I A
IV. Hitaji la maandalizi ya nia katika kutafsiri Biblia: uwe tayari kutendea kazi Neno la Mungu.
A. Uwe mtendaji wa Neno, Yakobo 1:22-25, taz. Ezra 7:10.
1. Sikiliza sauti ya Bwana unapojifunza Neno la Mungu, Ebr. 3:7-13.
2. Tekeleza maongozi ya Mungu haraka iwezekanavyo.
1
3. Usiwe na tabia ya kuwasomea wengine badala ya kusoma ili kumsikia Mungu akisema nawe .
4. Tarajia Neno la Mungu liathiri maisha yako, si tu mazoea yako ya kujifunza.
B. Hekima huja kwa kutii Neno la Mungu , si kulitafsiri tu, Zab. 111:10.
1. Wasomi hodari wa Biblia hawaishi kujifunza , badala yake, wanajifunza ili kuishi .
a. Kumbukumbu 4:6
b. Yoshua 1:7-8
2. Tunapata ufahamu wa Neno la Mungu kwa kulitafakari, na si kwa kuandika tu maelezo na sentensi chache, Zab. 119:98-101.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker