Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

Mwongozo wa Mkufunzi

Kutafsiri Biblia Kulingana na ushahidi wa wazi wa maandiko yenyewe, Mungu huwaandaa wawakilishi wake kupitia Neno la Mungu lililopuliziwa na Roho, Maandiko. Kila mtu ambaye Mungu anamwita katika huduma lazima adhamirie kujinidhamisha ili aweze kuwa mahiri katika Neno, kutii maagizo ya Neno, na kufundisha kweli ya Neno la Mungu. Kama mtenda kazi, lazima ajitahidi kutumia kwa halali Neno la kweli, na hivyo kukubaliwa na Bwana katika jitihada zake za kujifunza (2 Tim. 2:15). Katika kozi hii tunaangazia hitaji la ufasiri wa kibiblia, na kile kinachohitajika ili kutekeleza kazi hii kuu. Tutachunguza viwango vya kimungu na vya kibinadamu vya Biblia, na kutambulisha mbinu mwafaka ya ufasiri wa kibiblia iliyoundwa ili kukusaidia katika jitihada zako za kujifunza Maandiko ili kuziba pengo kati ya ulimwengu wa kale na wa sasa. Zaidi ya hayo, tutaangazia umuhimu wa aina za fasihi katika ufasiri wa Biblia, na kuchunguza aina nyingi za zana thabiti za marejeo za kitaaluma tunazoweza kuzipata tunapojaribu kuelewa maana ya Maandiko ya Biblia.

Mchungaji Dkt. Don L. Davis, (Ph.D., Chuo Kikuu cha Iowa) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry, ambayo ni huduma ya World Impact. Pia anahudumu kama Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact. TUMI imejitolea kuwezesha vuguvugu za upandaji makanisa kote ulimwenguni ambazo zinawaandaa viongozi ili kuendeleza Ufalme miongoni mwa watu maskini wa mijini. World Impact ni shirika la kimisheni la Kikristo ambalo limejidhatiti kuwezesha harakati za upandaji makanisa kwa njia ya kufanya uinjilisti, kuandaa na kuwawezesha maskini katika miji ya Amerika. Maono yetu ni kusajili, kuwezesha, na kuwatuma viongozi wa mijini ambao watapanda makanisa na kuzindua harakati za upandaji makanisa ya kienyeji.

kuandaa viongozi. kuwezesha harakati.

THE URBAN MINISTRY INSTITUTE • HUDUMA YA WORLD IMPACT, INC.

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker