Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 3 3 1
K U T A F S I R I B I B L I A
kwa ajili ya kazi ya huduma na ya Ufafanuzi wa Maandiko yanatakiwa yawe yameshakusanywa kwako. Kwa wale ambao watakuwa wamechelewa kukusanya ni muhimu iangaliwe namna na kiasi gani cha maksi ambacho unaweza kupunguza katika matokeo ya mwisho ya mwanafunzi husika. Hapa, busara yako kuhusiana na kazi hizi zilizocheleweshwa ndio itakayoamua kama utawapunguzia wanafunzi alama, jambo ambalo litasababisha mabadiliko katika madaraja yao ya mwisho. Kwa mwanafunzi mwenye udhuru ambao haukwepeki na ambao wewe mwenyewe unautambua, basi unaweza kutoa maelekezo kuhusiana na muda unaompa mwanafunzi ili akamilishe kazi yake. Hata hivyo, unaweza kutengeneza utaratibu wako kilingana na kazi zao, kumbuka kwamba lengo la msingi la kozi hizi sio kuhusu madaraja ambayo wanafunzi wanayapokea bali ni ile lishe ya kiroho na mafunzo ambayo kozi hizi zinatoa. Pia, kumbuka kwamba kuwasaidia wanafunzi wetu kufikia katika ubora pia ni sehemu ya muhimu zaidi ya mafunzo yetu.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker