Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

3 3 0 /

K U T A F S I R I B I B L I A

mafundisho kuhusu Yesu wa Nazareti kama mwokozi na Bwana kwa njia ya uchunguzi wetu wenyewe tunaoufanya kwenye kifungu cha andiko. Kile ambacho kinatakiwa kutazamwa kwa umakini hapa ni kama shauku ya kuhakiki andiko kwa kujifunza kwetu wenyewe ina msukumo wa kiburi (kwa sababu ya nia isiyo sahihi) au haiwezekani (kwa sababu ya ukosefu wa ujuzi wa kitaalamu na wa Biblia). Mungu kwa njia ya Mwandishi Luka anashughulika na madai haya yote mawili, na anasema kwamba shauku ya waberoya kuuchunguza ushuhuda wa Paulo na Sila kuhusiana na Maandiko haikuwa yenye kiburi wala majivuno. Ilikuwa yenye kicho na heshima! Wakumbushe wanafunzi wako juu ya wajibu wao mtakatifu wa kuuishi wito wao wa kuwa watoto wa Ibrahimu, na kuishi kama waamini katika ahadi takatifu za Mungu katika Maandiko. Kwa kweli, hakuwezi kuwa na motisha kubwa zaidi ili kuwa mwanafunzi wa Neno zaidi ya kuwa mkweli kwenye imani binafsi, wito binafsi na moyo wa kufanya hilo, kujitoa binafsi kikamilifu kwenye kweli kama tulivyoisikia katika ujumbe wa Yesu wa Nazareti. Aina ya maswali ya kuyapitia yameelekezwa moja kwa moja kwenye video hii na ile inayofuata kuhusu kupata ufahamu wa jumla wa matumizi ya zana, yaani zana hizo ni nini, nini lengo kuu katika kutafsiri Biblia, na tunawezaje kuzitumia kwa ufasaha ili kupata manufaa makubwa. Hakikisha wanafunzi wako wanaelewa kwamba kama wakitumia zana hizi kwa ufasaha, ufahamu wao juu ya Maandiko unaweza kufikia hatua mpya kabisa na yenye kina kirefu cha maarifa, usahihi, na manufaa makubwa. Sio tu kubadilishwa katika kujifunza kwao lakini, katika umuhimu uleule, kuhubiri kwao, kufundisha kwao na kuwasilisha Injili vilevile kutaimarishwa kwa kiasi kikubwa. Hongera, sasa umemaliza ile sehemu muhimu katika kazi yako kama mkufunzi! Hata hivyo, kwa namna nyingine, majukumu yako kama mkufunzi na msahihishaji ndio yanaanza sasa. Kazi yako ya kwanza kwa sasa ni kupangilia na kuratibu mazoezi na kazi za wanafunzi, na kuhakikisha kwamba unakusanya na kuweka madaraja kwenye mazoezi mbalimbali yaliyokusanywa mwishoni mwa kozi. Mpaka sasa maazimio

 3 Page 192 Maswali kwa

Wanafunzi na Majibu

 4 Page 218 Kazi

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker