Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

1 0 8 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Grenz, Stanley J., and John R. Franke. Beyond Foundationalism: Shaping Theology In a Postmodern Context . Louisville, KY: Westminster John Knox Press, 2000. Stuart, Douglas K. Old Testament Exegesis: A Handbook for Students and Pastors . 3rd Ed. Louisville, KY: Westminster John Knox Press, 2001. Traina, Robert A. Methodical Bible Study . Grand Rapids: Zondervan Publishing Company, 1985. Huduma yoyote halali ya Ufalme ina msingi wake katika kutendea kazi Neno lenye pumzi ya Mungu, yaani maandiko. Kama tulivyoona kwa Ezra katika kipengele chetu cha ibada, uwezo wako wa kusoma Sheria ya Bwana na kuitenda ndio ufunguo wa kukuwezesha kufundisha Kweli ya Mungu katikati ya watu wake, Kanisa, na kwa wale wasioamini. Kila eneo na hatua ya huduma inahusiana moja kwa moja na umahiri wako wa Neno la Mungu, na utayari wako wa kuruhusu Neno hilo kukutawala! Chukua muda wa kutafakari juu ya viwango vya huduma yako ya sasa nyumbani, kazini, kanisani na katikati ya jamii, na umwombe Roho Mtakatifu akuonyeshe namna ambavyo tafsiri na matumizi yako ya Neno yanaweza kuongeza na kukuza kwa kiwango fulani maisha na ushuhuda wako. Mwombe Bwana akufunulie maeneo fulani ya maisha na huduma yako ambayo yanahitaji nguvu za Neno lake ziwe halisi zaidi na zifanyike kipaumbele chako muhimu zaidi, na uwe tayari kubadilisha mtazamo au tabia yako katika hali yoyote ile ambayo Roho atakufunulia. Newbigin anasema kuna njia moja tu ambayo watu wa Mungu wanaweza kuifanya Injili iaminike: “ jibu pekee, hemenetiki pekee ya Injili , ni kusanyiko la wanaume na wanawake wanaoiamini na kuiishi . . . wana uwezo wa kutimiza kusudi lao kwa vile tu wamekita mizizi na kurudi katika ushirika wao kama jamii ya waamini.” Hizi eklesia [kanisa, kusanyiko] za watu halisi, katika maeneo halisi, wanaoshughulika na masuala halisi, na wenye ufahamu juu uhalisia wa maisha ya mwanadamu, kama Calvin alivyosema, ni udhihirisho “halisi” wa Kristo duniani kama ilivyo jumuiya ya Mungu mbinguni. ~ Gareth Weldon Icenogle. Biblical Foundations for Small Group Ministry . (electronic ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1994. Tunatumia Neno la Mungu katika jamii ya waaminio.

Kuhusianisha somo na huduma.

2

Ushauri na maombi.

page 321  4

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker