Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
1 1 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Katika somo hili tumechambua Mbinu ya Hatua Tatu ya kutafsiri Biblia, njia iliyokusudiwa kuchukulia kwa uzito maana ya kifungu cha Biblia katika muktadha wake wa asili na wa kwanza, kugundua kanuni za Biblia zilizomo ndani ya kifungu husika, na kisha kutumia kwa bidii kanuni hizo katika maisha yetu kwa imani na utii tukiwezeshwa na Roho Mtakatifu. Sasa, katika somo letu linalofuata, tutaelekeza fikira zetu katika umuhimu wa tanzu, au aina za fasihi, tunapotumia mbinu hii ya kutafsiri Biblia katika kushughulika kwetu na vitabu hivi vya aina mbalimbali, vilivyojaa utajiri, na vya ajabu vya maktaba yetu takatifu, yaani Neno la Mungu. Tutatoa maelezo kwa ufupi kuhusiana na manufaa yanayotokana na kuzingatia elimu ya tanzu, na kuangazia baadhi ya dhana muhimu ambazo ni msingi wa aina hii maalum ya hemenetiki.
Kuelekea somo linalofuata.
2
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker