Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

1 3 0 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Fasihi ya hekima ni muhimu sana kwa sababu inajishughulisha na masuala ambayo ni muhimu sana katika maisha yetu bila kutatua mivutano yote na matatizo yanayohusiana nayo. Imekusudiwa kuinua roho zetu katikati ya maisha, sio kutoa majibu ya mwisho katika masuala ya maisha. F. Kazi za kishairi – muundo wa utanzu wa kibiblia ambao kwa kawaida huonekana katika muundo wa wimbo, soneti, au tenzi, na imeundwa kuonyesha ukweli katika maana yake halisi ili kutugusa kihisia na kututia moyo.

1. Inahusishwa kwa karibu na utamaduni wa muziki wa Kiebrania.

2. Mita, mdundo, na kasi ni muhimu kwa mashairi kama vipande vya kisanii.

3

3. Namna nyimbo zilivyoandikwa ni muhimu pia katika suala la kutambua kilichoandikwa.

4. Zaburi ndio mgodi tajiri zaidi wa ushairi unaopatikana katika Agano la Kale, lakini ushairi unapatikana kote katika Biblia, hasa katika Fasihi ya Hekima.

5. Nyimbo zilikuwa sehemu muhimu ya maisha na utamaduni wa Kiebrania (k.m., Wimbo wa Kisima, Hes. 21:17-18; Mwa. 31:27; Yer. 7:34, nk.).

6. Mashairi mengi yalisindikizwa na ala za muziki (Kut. 15:20; Isa. 23:16).

7. Ushairi wa Kiebrania ulikuwa aina ya mawasiliano iliyokaririwa, ikionyesha lafudhi ya vokali na mikazo (huu ndio ufunguo wa mita yake).

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker