Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

1 4 8 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Umoja NA Utofauti wa Maandiko

Kwa ufupi, umoja na utofauti wa maandiko ni lazima utambuliwe na kuwekwa katika mizani makini. Usomi mwingi wa kiliberali huelekea kuzingatia zaidi utofauti kiasi cha kufunika kabisa dhana ya umoja. Usomi mwingi kihafidhina huelekea kuzingatia sana umoja kiasi cha kuondoa dhana ya utofauti. Pasipo kutambua umoja wa maandiko, kanoni ya Biblia kwa ujumla haiwezi kufanya kazi kama msingi wenye mamlaka wa imani na maisha ya Kikristo kama ilivyofanya katika historia. Pasipo kuthamini utofauti unaotokana na kusikia kila andiko, kitabu na mwandishi kwa namna yake mwenyewe, kuna uwezekano hatarishi wa kufasiri maandiko kimakosa na kutotambua kile ambacho Mungu alikusudia kuwaambia watu wake wakati wowote katika historia yao. Kitheolojia, umoja wa maandiko huweka wazi mipaka ya mawazo na tabia ambayo watu binafsi au ‘makanisa’ hayawezi kuitwa kihalali kuwa ya Kikristo endapo wataivuka. Kwa upande mwingine, utofauti wa maandiko huonyesha namna ambavyo hakuna dhehebu moja au mapokeo ya kikanisa yaliyo na hakimiliki ya ukweli. Mtu anaweza kuwa mzushi kwa kuwa na fikra pana kupitiliza au finyu mno! ~ C. L. Blomberg. “The Unity and Diversity of Scripture.” The New Dictionary of Biblical Theology . T. D. Alexander, ed. (electronic ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001.

3

III. Unabii kama tanzu ya fasihi ya Biblia.

A. Unabii unawasilisha ukweli kuhusu Mungu na ulimwengu.

1. Unashughulika na maswali makuu ya uwepo wa mwanadamu na maisha yake.

2. Unashughulika na asili ya uumbaji na ulimwengu.

3. Unatokana na mtazamo wa ulimwengu nje ya fahamu (yaani, Mungu wa Utatu anayefanya mapenzi yake ulimwenguni).

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker