Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 5 9

K U T A F S I R I B I B L I A

MUUNGANIKO

Somo hili linalenga katika nafasi na matumizi ya tanzu katika ufasiri wa Biblia. Dhana zifuatazo hapa chini ni muhtasari wa maarifa makuu yaliyotolewa katika sehemu hii kuhusiana na umuhimu wa tanzu katika hemenetiki maalum. ³ Neno “tanzu” linarejelea muundo maalum wa fasihi ambao umetumika kuwasilisha ukweli na lazima utafsiriwe kulingana na kanuni za muundo huo. ³ Kazi ya kutafsiri Biblia kwa kuzingatia matumizi ya tanzu lazima ianze kwa ufahamu makini wa dhana za msingi za elimu ya tanzu, ambayo inathibitisha ukweli kwamba Biblia yenyewe ni kitabu cha fasihi, ambacho kimepangiliwa kwa umakini mkubwa na kinapaswa kutafsiriwa kwa kuongozwa na kanuni za fasihi kama vitabu vingine vya fasihi, na kwamba Mungu alitumia aina na mbinu za kifasihi za kibinadamu ili kuwasilisha Neno lake kwetu. ³ Kuna aina na miundo mingi muhimu ya fasihi katika maandiko. Hizi ni pamoja na matumizi ya simulizi (za kihistoria na za kutunga), Sheria (maandiko ya kisheria), nyaraka (barua), unabii, fasihi ya hekima (methali, monolojia, vitendawili, hekaya, mafumbo, istiari, n.k.), na uwepo wa kazi za kishairi. ³ Tanzu hutokea kwa sababu ya madhumuni mahususi ya kifasihi ya waandishi ya kushughulikia mahitaji na masuala mahususi kwa hadhira zao husika, na pia kuongeza uelewa wetu wa msingi wa maisha ya mwanadamu. Elimu juu ya tanzu pia hutuwezesha kuufahamu ukweli kwa kuuona ukiwasilishwa katika muundo wake halisi, na pia kuonyesha ustadi wa waandishi wa Biblia kama walivyoongozwa na Roho, na kufunua utajiri wa siri ya Mungu na kazi yake katika dunia. ³ Kuzingatia kwa umakini matumizi ya tanzu na kanuni za kuzitafsiri kunaweza kutupatia manufaa makubwa katika jitihada zetu za kutafsiri Biblia; ufahamu kuhusu tanzu unaweza kutuwezesha kugundua nia ya asili ya mwandishi, kutujenga tunapotambua maana ya maandiko kwa ajili ya maisha yetu, kututajirisha na kutuburudisha kupitia uzuri wa maandiko yenyewe, na kututia nuru kupitia ujuzi wa kusudi na mapenzi ya Mungu. ³ Neno “Hemenetiki maalum” linazungumzia sheria na taratibu maalum zinazotuwezesha kufasiri aina za fasihi ya Biblia. ³ Simulizi ndio aina ya tanzu iliyoenea zaidi katika maandiko, na inajumuisha hadithi na simulizi za hadithi ambazo ni za kihistoria na zilizotungwa (za kufikirika).

Muhtasari wa Dhana Muhimu

3

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker