Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 6 1

K U T A F S I R I B I B L I A

Kama mwanafunzi wa Neno la Mungu, utahitaji kushughulika na kanuni, sheria, na taratibu ili uweze kuelewa kikamilifu na kutumia maarifa ya somo hili kuhusiana na tanzu za Biblia. Uwezo wako wa kuelewa dhana hii na kuitumia katika jitihada zako za kujifunza Biblia utaathiri mwenendo wako wote na huduma yako, hasa mahubiri na mafundisho yako, na jitihada zako binafsi za kujifunza Biblia. Sasa unahitaji kutafakari kwa kina yale maswali kuhusu tanzu ambayo yamedumu akilini mwako wakati wote wa majadiliano na mchakato mzima wa kujifunza somo hili. Tumia maswali yafuatayo hapa chini ili kukusaidia kuchambua na kufafanua yale maeneo ambayo bado hayajaridhisha katika ufahamu wako juu ya nafasi na umuhimu wa elimu ya tanzu katika mchakato wa kutafsiri Biblia. * Je, sasa unaamini kwamba Biblia haiwezi kufasiriwa ipasavyo bila kuelewa kwa umakini kuhusiana na tanzu za Biblia? Je, unaamini kwamba kwa sababu Biblia yenyewe ni kitabu cha fasihi, basi ni lazima tutafute kuifasiri kulingana na sheria na kanuni za kifasihi kama ilivyo kwa kazi nyinginezo za fasihi? Elezea jibu lako. * Kati ya tanzu zilizoorodheshwa katika somo hili, ni ipi imekuwa changamoto kubwa kwako kuelewa, kutumia, na kufundisha kwa wengine? (Kumbuka, hizi ni pamoja na simulizi, Sheria, nyaraka, unabii [na fasihi ya apokaliptiki], fasihi ya hekima, na kazi za kishairi). * Je, umetumia muda mwingi katika kujifunza kuhusu tanzu? Umekuwa na maoni gani kwa ujumla juu ya hilo? Je, somo hili limeleta tofauti yoyote katika mtazamo wako kuhusu umuhimu wa elimu ya tanzu katika jitihada zako binafsi za kujifunza Biblia? Eleza. * Kwa nini ni muhimu kutumia Mbinu ya Hatua Tatu katika kujifunza kwako aina mahususi za tanzu, na kanuni za kuzitafsiri? Je, kuna aina za tanzu ambazo hazitafsiriwi kwa kutmia Mbinu ya Hatua Tatu ? Eleza. * Unatumia muda gani kujifunza hadithi na unabii wa Biblia? Kwa kuzingatia ukweli kwamba aina hizi mbili za tanzu zinaunda sehemu kubwa ya maudhui ya Biblia, je, unadhani kuna namna unapuuzia au unazingatia elimu hii unapojifunza Biblia wakati huu? * Kuna aina fulani ya utanzu wa kibiblia ambao wewe binafsi una mwelekeo wa kuizingatia zaidi? Kwa nini unadhani unaweka mkazo wako katika aina hii ya fasihi ya Biblia – ni rahisi kuelewa, ina kuvutia zaidi, au una sababu nyingine? * Unatumia muda gani kusoma Injili na mifano iliyomo? Unadhani endapo ungeelewa vizuri zaidi “namna simulizi zinavyofanya kazi” ungetumia

Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi

3

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker