Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 7 3

K U T A F S I R I B I B L I A

yote kwa ajili ya kuthibitisha ukweli unaotuweka huru kwa mujibu wa Neno la Bwana (Yohana 8:31-32).

Baada ya kutamka na/au kuimba ukiri huu wa Imani ya Nikea (ona kiambatisho), omba maombi yafuatayo: Ee Mungu, kwa Roho wako, utuambie tunachohitaji kusikia, na utuonyeshe kile tunachopaswa kufanya ili kumtii Yesu Kristo Mwokozi wetu.

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

~ Presbyterian Church (U.S.A.) and Cumberland Presbyterian Church. The Theology and Worship Ministry Unit. Book of Common Worship . Louisville: Westminister/John Knox Press, 1993. p. 60.

Weka kando vitabu vyako na zana zote za kujifunzia (isipokuwa Biblia), kusanya mawazo na ufahamu wako, na ufanye jaribio la Somo la 3, Fasihi ya Kibiblia: Kutafsiri Tanzu za Biblia .

Jaribio

Mazoezi ya Kukariri maandiko

Pitia na mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita, yaani 2 Timotheo 3:14-17.

4

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yani hoja kuu ambazowaandishi walikusudia kuziwasilisha.

Kazi ya kukusanya

MIFANO YA REJEA

Zana zinazofaa kwa moyo wenye njaa.

Wale wanaoshikilia mtazamo sahili wa Biblia (yaani, wanaelekea kupuuza mtazamo wa kwamba Biblia ni fasihi, na kwamba kuitafsiri kunapaswa kuzingatia sheria na kanuni za fasihi) huchukulia mkazo wowote juu ya elimu wa tanzu na utumiaji wa zana za kitaalamu kuwa zoezi gumu sana na lenye mwelekeo wa uanazuoni, na kwamba zoezi hilo ni kwa ajili ya watu wachache tu wanaoweza kuelewa kanuni zote za kifasihi na kumudu gharama za kumiliki zana zote hizo za kitaalamu. Wana wasiwasi, kwa namna iliyo halali kabisa, kwamba Biblia “inafichwa”mbali na mtu wa kawaida ambaye anapenda tu na kumwamini Bwana Yesu na kuwa mfuasi wake, na anayetafuta kusoma Neno la Mungu kwa nia ya kuliamini na kulitii. Wao si wasomi wa Kiyunani, na hawataweza kamwe kuelewa kanuni na sheria zote za Biblia kama

1

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker