Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 1 7 7
K U T A F S I R I B I B L I A
• Bila kujali ni zana ipi tunayotumia, tunapaswa kutumia rejea hizi kwa wingi, lakini daima hatupaswi kusahau kwamba matumizi sahihi ya zana hizi ni yale yanayotoa mwanga zaidi kuhusiana na maana ya maandiko, na sio kukanusha au kudhoofisha umuhimu wake.
I. Umuhimu wa zana katika Ufasiri wa Biblia.
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
A. Kusudi lake: kusaidia kuziba pengo kati ya ulimwengu wa Biblia na ulimwengu wetu wa sasa.
Daima kuna haja ya ufasiri
Kitendo cha maandiko kujithibitisha yenyewe kuwa ya kweli hakutupi uhakika kwamba tafsiri zote ni kweli. Wafasiri wa kibinadamu wanaweza kufanya, na wamefanya makosa mengi. Kwa sababu hiyo maana za maandiko zimezua utata katika maeneo mengi muhimu na yasiyo muhimu sana. ~ E. J. Schnabel. “Scripture.” New Dictionary of Biblical Theology. T. D. Alexander, ed. (electronic ed.). InterVarsity Press: Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001.
1. Mbinu ya Hatua Tatu imejikita katika kuunganisha ulimwengu wa kale na ulimwengu wetu wa sasa.
2. Ili mbinu hiyo ifanye kazi ipasavyo, ni lazima tujitahidi kuelewa maana ambayo waandishi wa Biblia waliikusudia katika muktadha wao wa asili.
4
3. KatikaufasiriwaBiblia, zanahizi nimuhimu sana katika kutuunganisha na nahau, tamaduni, lugha, na matukio ya kihistoria yanayohusiana na ulimwengu wa Biblia (yaani, “Unakuwepo”).
B. Fursa yake: kumekuwa na mlipuko wa nyenzo nyingi za kibiblia tangu miaka ya 1950.
C. Faida yake : uaminifu kwa ujumbe wa Neno la Mungu kwa kufuata masharti na kanuni za Neno lenyewe.
1. Kuelewa muktadha asilia.
2. Kuweza kubainisha na kugundua maana za matini kama ambavyo hadhira asilia ingeuelewa ujumbe husika .
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker