Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 1 8 1
K U T A F S I R I B I B L I A
c. Ilizungumzwa sana naWayahudi katika siku za Yesu na yawezekana ndiyo lugha iliyozungumzwa na Yesu katika mazungumzo ya kawaida. Ilipendelewa na Wayahudi kwa sababu ilikuwa na mizizi ya Kisemiti (ilifanana na Kiebrania) lakini ilieleweka kwa kawaida na watu wengine wengi. Katika siku za Yesu, lilikuwa jambo la kawaida kusoma maandiko katika Sinagogi katika Kiebrania na kuyasoma katika Kiaramu ili watu wasiozungumza Kiebrania waelewe. Kuanzia takriban mwaka 200 K.K. sehemu za maandiko ya Kiebrania zilianza kuandikwa katika Kiaramu katika vijitabu vilivyoitwa “Targum.”
3. Kiyunanii
a. Lahaja ya Koine – (“Kiyunani cha mitaani”) tofauti na sarufi ya Kiyunani cha kawaida, ni rahisi na inaeleweka zaidi.
b. Ni lugha rahisi, maarufu, lugha ya kawaida ya biashara na serikali katika ufalme wa Kirumi ulioenea.
4
c. Tafsiri ya 70 ( Septuagint ) – tafsiri ya maandiko ya Agano la Kale katika Kiyunani iliyofanywa na wasomi 70 wa Kiyahudi. (Mara nyingi inaitwa kwa kifupi LXX ambayo ni namba 70 kwa lugha ya Kirumi).
B. Changamoto ya tafsiri ya lugha: kwa nini tafsiri ni ngumu kufanya?
1. Kushinda tofauti za maana matumizi, na sarufi ya maneno.
a. Tafsiri inahusu utamaduni unaopokea; lakini inakuwaje ikiwa utamaduni unaopokea una chaguzi chache au tofauti na zile zilizoorodheshwa katika maandiko?
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker