Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 8 3

K U T A F S I R I B I B L I A

C. Changamoto za kutafsiri: kuwa mwaminifu kwa ujumbe wa maandiko na kwa lugha na kanuni za kitamaduni za utamaduni unaopokea.

1. Watafsiri huchagua mbinu tofauti katika falsafa zao za tafsiri.

a. Tafsiri Sisisi – maneno halisi (kihalisi iwezekanavyo), karibu iwezekanavyo na muundo asilia wa kisarufi.

b. Ulinganifu thabiti – maana kamili kwa kutumia maneno yoyote yanayoweza kupatikana ili kubeba maana hiyo.

2. Watafsiri wenyewe wanatofautiana sana (yaani, wana imani tofauti kuhusu kuaminika kwa maandiko).

a. Wahariri wa Biblia ya Dartmouth walijisikia huru kuhariri maandiko, wakihifadhi tu yale waliyoona kuwa yasiyo ya kurudiwa rudiwa na ya lazima zaidi.

4

b. Mashahidi wa Yehova wamechapisha toleo lao la Biblia kwa sababu baadhi ya sehemu zinaonekana kutokubaliana na mafundisho yao. Kwa hiyo, wamebadilisha sehemu hizo.

c. Jerusalem Bible ni tafsiri nzuri sana ya Kikatoliki lakini maelezo yanayoambatana na Biblia hiyo yanafasiri matini hayo kwa mtazamo wa kiutamaduni wa Kikatoliki.

3. Watafsiri hufanya kazi peke yao au katika kamati (yaani, vikundi vya wasomi huwa na ujuzi kamili zaidi na lazima viwe na usawaziko wa kutosha ili maoni ya kila mtu yasikike).

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker