Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 9 5

K U T A F S I R I B I B L I A

Uhakiki wa “Juu” na wa “Chini” wa Biblia: Tofauti ni nini?

[Uhakiki wa juu ni] sehemu ya utafiti wa kibiblia ambao hujaribu kutathmini vipengele vya utunzi kama vile tarehe ya kuandikwa, uandishi, hadhira, vyanzo vilivyotumiwa katika uandishi (vya mdomo, maandishi, n.k.), na muundo wa jumla wa fasihi (ikiwa ni pamoja na kulinganisha na vipengele na mitindo ya kisasa ya fasihi isiyo ya kibiblia); haya yote yakifanyika kwa njia ya kujenga na kwa mtazamo wa juu wa uadilifu wa maandiko, eneo hili la elimu linaweza kutoa michango muhimu; yakifanyika pasipo kuwa na kicho na hesima kwa maandiko, linaweza kuleta ushawishi wa uharibifu; kwa hivyo, kwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita, neno hili wakati mwingine linatumika katika mitazamo ya kimantiki juu ya Biblia, ambayo ilielekea kuiona tu kama kazi ya kibinadamu, si kama ufunuo mmoja kutoka kwa Mungu; [linganisha hili na] uhakiki wa chini (= uhakiki wa kimaandishi), ambao unahusika na kuthibitisha matini bora zaidi za maandiko za kufanyia kazi. ~ Paul Karleen. The Handbook to Bible Study . (electronic ed.). New York: Oxford University Press, 1987.

I. Visaidizi vya rejea mtambuka, Biblia za mada, Biblia za rejea mtambuka, na konkodansi za mada.

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

4

A. Zana za rejea mtambuka (zinasaidia katika hatua ya kupata kanuni za jumla).

1. Ufafanuzi: Visaidizi vya rejea mtambuka hutusaidia kupata miunganiko kati ya maandiko ya Biblia yenye mada moja au zinazohusiana kwa kulinganisha maandiko na maandiko.

2. Mapendekezo ya visaidizi vya rejea mtambuka.

a. The New Treasury of Scriptural Knowledge , Jerome H. Smith, ed. (Thomas Nelson 1997)

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker