Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 9 7

K U T A F S I R I B I B L I A

3. Manufaa: zinaokoa wakati mno katika kutafuta matini husika zenye mada moja.

4. Tahadhari: kutegemea sana zana hizi kunaweza kufanya uchambuzi wa mtu kuwa tofauti kidogo na usio na muunganiko (kuzingatia sehemu na sio mada na vitabu vya Biblia nzima).

II. Kamusi za Biblia, ensaiklopidia za Biblia, atlasi za Biblia, na kazi za rejea za historia na desturi za Biblia.

Ulinganishi wa Imani: Tumia maandiko kufasiri maandiko Kila kitabu kilitokana na chazo kile kile cha ufahamu wa kimungu, ili kwamba mafundisho ya vitabu sitini na sita vya Biblia yakamilishane pasipo kukinzana. Ikiwa bado hatuwezi kuona hili, kosa liko ndani yetu, si katika maandiko. Ni hakika kwamba maandiko hayapingani popote; badala yake, kifungu kimoja kinaelezea kingine. Kanuni hii nzuri ya kufasiri maandiko kwa maandiko wakati mwingine huitwa mlinganisho wa maandiko au ulinganishi wa imani. ~ J. I. Packer. Concise Theology: A Guide to Historic Christian Beliefs. (electronic ed.). Wheaton, IL: Tyndale House, 1995.

A. Kamusi ya Biblia, ensaiklopidia ya Biblia

1. Maelezo: ni kwa ajili ya kutoa usuli juu ya historia, utamaduni, desturi za kijamii, watu, topografia, na mambo yanayohusiana ya nyakati za Biblia .

2. Ni visaidizi vya pekee sana katika kuziba pengo la kihistoria na kiutamaduni kati ya ulimwengu wetu na ulimwengu wa kale.

4

a. Zana hizi ni zana muhimu zaidi za kufupisha umbali kati ya ulimwengu wetu na ulimwengu wa Biblia!

b. Zina vitabu vingi na zanatepe ( software ) nyingi, bora, na zinazopatikana kwa urahisi.

3. Zinafaa katika kutambua taarifa juu ya dhana muhimu za kibiblia.

a. Watu (Abrahamu, Senakeribu, Ruthu).

b. Maeneo (Uru, Bethlehemu, Gosheni, Bahari ya Galilaya, Ashuru).

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker