Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
5 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
³ Tunaandaa mioyo yetu kwa njia ya kunyenyekea na maombi, bidii na kudhamiria, na kujighulisha kwa bidii katika Neno la Mungu kama mtenda kazi. Tunaandaa akili zetu kwa kuchukua majukumu ya mpelelezi, mtafiti, na mwanasayansi – kuchunguza Neno kwa bidii, kufuatilia kwa ukaribu mawazo mbali mbali, na kupima kila ushahidi kwa umakini kabla ya kutoa hitimisho. Tunaandaa nia zetu kwa kulitii Neno, si kulisikia tu; na kwa kukumbatia ukweli kwamba hekima inatokana na kuitikia Neno la Mungu, si kulitafakari tu. ³ Maandiko yanasema kwa uwazi na kwa ujasiri kwamba Neno la Mungu limevuviwa na Mungu, “limepuliziwa na Mungu,” kupitia nguvu na kazi ya RohoMtakatifu. Biblia ni kitabu kinachotokana na uandishi wa kibinadamu na uvuvio wa kimungu, hata hivyo hakuna andiko linalotokana na tafsiri yoyote ya matakwa ya mtu binafsi, bali waandishi “waliongozwa” na Roho Mtakatifu. ³ Kuna nadharia tano kuu za uvuvio zinazolenga kueleza jinsi Roho Mtakatifu alivyowaongoza kwa usahihi waandishi wa maandiko. Hizi ni pamoja na Nadharia ya Uvuvio wa Kiimla , Nadharia ya Uvuvio wa kihisia au uwezo wa usili , Nadharia ya Kuangaziwa, Nadharia ya uvuvio wa sehemu, na Nadharia ya Uvuvio wa neno kwa neno au Uvuvio Kamili . Nadharia ya Uvuvio wa neno kwa neno au Uvuvio Kamili ni imani ya kwamba maandiko yote ya Biblia, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa maneno aliyoyachagua mwandishi, ni matokeo ya uongozi na uchaguzi wa Mungu. ³ Uhakiki wa kisasa wa Biblia unajaribu kufuatilia asili ya maandiko kwa kuanzia na matukio ya awali yanayonenwa katika Biblia hadi simulizi halisi za matukio hayo yaliyorekodiwa katika vitabu vya kikanoni vya maandiko. Uhakiki huu unalenga kufuatilia ujumbe wa Mungu tangu tukio halisi lililorekodiwa na muktadha wake hadi tafsiri ya maandiko tuliyo nayo leo. ³ Vipengele muhimu vya uhakiki wa kisasa wa Biblia vinahusisha uhakiki wa muundo (kufuatilia mapokeo simulizi), uhakiki wa chanzo (kutafuta vyanzo vya maandiko), uhakiki wa lugha (lugha, maneno, na sarufi), uhakiki wa maandishi (nakala za maandishi), uhakiki wa kifasihi (kanuni za fasihi), uhakiki wa kikanoni (jinsi vitabu vilivyochaguliwa), uhakiki wa uandishi (madhumuni ya waandishi), uhakiki wa kihistoria (historia na utamaduni), na uhakiki wa tafsiri. ³ Licha ya madai yanayotolewa na wasomi wengi leo, tunaweza kuwa na uhakika kwamba maandiko kwa kweli ni Neno la Mungu linaloishi na kudumu milele.
1
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker