Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

5 8 /

K U T A F S I R I B I B L I A

KAZI

2 Petro 1:19-21

Kukariri maandiko

Ili kujiandaa na kipindi, tafadhali tembelea: Www.tumi.org/books ili kupata kazi ya usomaji ya wiki ijayo au muulize Mkufunzi wako.

Kazi ya usomaji

Wiki ijayo, utaulizwa maswali kuhusu maudhui (yaliyomo kwenye video) ya somo hili. Hakikisha kwamba unatumia muda wa kutosha kupitia maelezo uliyoandika. Zingatia zaidi mawazo makuu ya somo. Soma maeneo uliyoagizwa, na uandike muhtasari usiozidi aya moja au mbili kwa kila eneo uliloagizwa kusoma. Katika muhtasari huo tafadhali eleza kile ambacho kwa uelewa wako kilikuwa wazo kuu la kila eneo au kitabu ulichosoma. Usijitaabishe kutoa maelezo mengi; andika tu kile unachoona kuwa wazo kuu linalozungumziwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali hakikisha unakuja na muhtasari huo darasani wiki ijayo. (Angalia “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” mwishoni mwa somo hili). Katika somo hili tulichunguza hitaji la ufasiri wa kibiblia, na umuhimu wa maandalizi yetu wenyewe ya mioyo yetu, akili zetu, na nia zetu ili kuliendea Neno la milele la Mungu Aliye Hai. Kama kitabu cha kimungu na cha kibinadamu, lazima tutegemee msaada wa Roho Mtakatifu ili kuelewa Neno la Mungu, na tuwe na utayari wa kuruhusu Neno hilo libadilishe maisha yetu kabla ya kulishirikisha kwa wengine. Katika sehemu yetu iliyofuata tulichunguza uvuvio na mamlaka ya Biblia, na kujadili nafasi ya uhakiki wa kisasa wa Biblia katika uelewa wa Neno la Mungu leo. Katika somo letu linalofuata tutaingia kwa undani zaidi kuangalia Mbinu ya Hatua Tatu ya ufasiri wa Biblia, njia rahisi lakini yenye ufanisi iliyobuniwa ili kutusaidia kuelewa kweli za maandiko na kuziba pengo kati ya ulimwengu wa kale na huu wa sasa. Mbinu hii inajumuisha matumizi yaliyojaa maombi na yenye nidhamu ya zana za kujifunza Biblia ili kutuwezesha kuuelewa ujumbe wa Mungu kwa hadhira asilia, kugundua kanuni za jumla kwa faida ya sasa, na kuzitumia maishani mwetu.

Kazi nyingine

1

page 315  9

Kuelekea somo linalofuata

Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia nyenzo hizi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha toka kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license.

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker