Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 0 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
³ Katika kujiandaa kutumia njia yoyote ya kujifunza Biblia, jambo kubwa na la msingi zaidi ni mtazamo wa mwanafunzi wa maandiko, kwa sababu hatua hizi za kujifunza kupitia Mbinu ya Hatua Tatu zinadai unyenyekevu, bidii, na uhuru katika kila hatua. ³ Kama watumwa wa haki chini ya ubwana wa Kristo, tumeitwa kulitii Neno lake katika kila nyanja ya maisha na huduma zetu, kwa hiyo, namna yoyote halali ya kutafsiri Biblia lazima ilenge katika kulifahamu Neno la Mungu kwa madhumuni ya kuleta badiliko katika maisha , na si habari ya kujaza taarifa akilini . ³ Mbinu ya Hatua Tatu ni mbinu bora ya kutafsiri Biblia ambayo inaweza kutumika vizuri katika kushughulika na migawanyo mbali mbali ya maandiko (maneno, aya, sura, vitabu, sehemu). ³ Kila kujifunza Neno la Mungu huanza na kunyenyekea kwetu kwa Roho Mtakatifu, ambaye peke yake ndiye mwandishi wa maandiko na ndiye pekee anayetosha kutufundisha maana na umuhimu wa maandiko katika maisha yetu leo. ³ Hatua ya kwanza katika kutumia Mbinu ya Hatua Tatu ni kuchunguza kwa undani yaliyomo katika andiko, kubainisha usuli (historia) wa kitabu, mwandishi wake na hadhira, madhumuni ya kuandikwa kwake, pamoja na namna lilivyotafsiriwa katika tafsiri mbalimbali. ³ Kupata kanuni za jumla za andiko au kifungu ni hatua ya pili ya Mbinu ya Hatua Tatu , na inahusisha kutafuta jumbe kuu, kweli, maagizo, au mafundisho yaliyomo katika kifungu. Hatua hii inahusisha kuangazia maana ya kifungu katika mazingira (muktadha) yake ya asili , na hatimaye kile ambacho kifungu kinamaanisha kwetu katika maisha yetu leo . Kanuni hizi lazima zielezwe waziwazi, zikilinganishwa na mafundisho mengine ya Maandiko Matakatifu ndani ya Biblia, na kufafanuliwa zaidi kwa faida ya kujifunza kwa kina na kulitumia Neno la Mungu kwa ufanisi zaidi. ³ Baada ya kuona maelezo na kuchota kanuni zilizomo katika maandiko, tunaenda kwenye hatua ya tatu ya Mbinu ya Hatua Tatu ambayo ni lengo letu la kutendea kazi kanuni za kiroho katika nguvu za Roho Mtakatifu. Kutendea kazi Neno ni kitendo cha kuelekeza moyo kwenye Kweli ya Neno la Mungu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu . Hili linahitaji uwezo wa kupambanua na utayari wa kutii mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker