Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 0 6 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Biblia yako katika lugha ya asili haitoshi!
(Kutokana na kisa cha kweli). Alipokuwa akikusanya kazi yake ya ufafanuzi (exegetical project) katika somo la kitabu cha Warumi, mwanafunzi mmoja aliambiwa na profesa wake (ambaye alikuwa amesahihisha kazi yake ya kwanza ya somo hilo) kwamba alikuwa amevunja kanuni za msingi katika kutumia zana za lugha. Profesa huyo alieleza hivi: “Huwezi kwenda kwenye kamusi ya kitheolojia au kamusi ya lugha na kudhania kwamba matumizi yote ya neno fulani yaliyoandikwa humo ndizo maana zilizokusudiwa mahali hapa . Hungetumia kamusi ya Kiingereza au Kihispania kwa njia hiyo; ungetafuta neno, ukapata ufafanuzi unaofaa katika muktadha wa kazi yako, na kisha utumie maana hiyo moja . Wewe umetumia maana zote za neno katika uandishi wako, na kwa sababu hiyo ukafanya makosa makubwa katika kazi yako.” Profesa huyo aliendelea kusema kwamba ni pale tu unapojua jinsi mwandishi mmoja-mmoja alivyotumia neno (kwa mfano, namna neno fulani lilivyotumiwa na Petro, Paulo, au Yohana katika uandishi wake wote) ndipo unaweza kuwa na uhakika kwamba unatumia vyanzo vyako vya lugha ipasavyo. Kwa kuwa Biblia iliandikwa katika Kiebrania, Kiaramu, na Kiyunani, na kwa kuwa wengi wetu hatujui lugha hizi, tunawezaje kuwa na uhakika kwamba tunasoma maandiko hayo ipasavyo? Je, tutatumiaje zana za lugha ikiwa hatujui kwa hakika namna mwandishi alivyotumia neno au kifungu cha maneno fulani? Mojawapo ya shida zinazo jitokeza kwa haraka kwa wale wanaogundua Mbinu ya Hatua Tatu ni kwamba wanaanza kutumia njia yao mpya waliyoigundua kuchambua maelezo mahususi ya sehemu nyingi za Biblia kana kwamba ni kifungu kimoja. Bila mwongozo wa jinsi ya kuunganisha na kuleta pamoja mawazo yao katika maana ya jumla ya maandiko, wanaibua idadi kubwa ya mada, jumbe, na masomo yasiyo na muunganiko na hawawezi kamwe kuyaleta pamoja chini ya mada moja inayoeleweka. Kwa maoni yako, je, maandiko yanamadamoja, yenyemuunganiko namtiririkommoja na ambayo ingeweza kutumika kama kiini cha mafunzo yetu yote na hivyo kuturuhusu kutafsiri mawazo yetu katika msingi wa mada hiyo kuu? Sisi kama wanafunzi wa Biblia, ni kwa namna gani tunweza kuepuka kujikitia katika maelezo ya kifungu kimoja kiasi kwamba tukapoteza “taswira kubwa,” ujumbe na maana pana zaidi ya Biblia yenyewe? Tunawezaje kuepukana na tatizo la msingi la Mafarisayo, ambao walifahamu kwa undani maandiko nukta kwa nukta lakini wakashindwa kabisa katika kuona mambo makuu ya maandiko na kuyatendea kazi katika maisha yao (yaani, waliweza kuona miti vizuri, wakashindwa kuona msitu). Tunawezaje kuiona Biblia katika ujumla wake na bado kupata faida pale tunapojifunza sehemu na vifungu vyake? Kushindwa kutofautisha matawi, miti na msitu.
3
2
4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker