Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 1 4 /
K U T A F S I R I B I B L I A
katika maandiko ni za kweli na sahihi, kwamba hadithi hizo zimeandikwa kwa ustadi na weledi wa sanaa, kwamba tunaweza kukutana na Mungu kupitia hadithi, na kwamba mara nyingi Mungu hutoa ufafanuzi wake mwenyewe kuhusu maana ya simulizi za hadithi za Biblia. • Kuelezea dhana muhimu za theolojia ya hadithi: kwamba hadithi hutuleta katika uwepo wa kisakramenti, ni muhimu zaidi kuliko maelezo ya kawaida, zinakubalika kama msingi wa maongozi katika jamii ya Wakristo, kwamba tamaduni za Kikristo hukua na kujifafanua zenyewe kwa njia ya hadithi, na kwamba hadithi hutangulia na kuzaa jumuiya, maonyo na uwajibikaji, na huzalisha theolojia, liturjia na sakramenti. Hadithi ni historia. • Kutaja na kuelezea vipengele vya jumla vya simulizi katika maandiko, ikijumuisha mazingira, wahusika, mtazamo wa mwandishi, mtiririko (ploti), na dhamira ya hadithi. • Kuelezea kanuni za jumla zinazohusu unabii kama aina ya tafsiri ya kibiblia, ikijumuisha jinsi unabii unavyowasilisha ukweli kuhusuMunguna ulimwengu, yakwamba unatiririka kutoka kwa Roho na ni njia maalum ya ufunuo kutoka kwa Mungu ambayo inajidhihirisha kupitia mtu au kwa njia ya fasihi. • kubainisha vipengele vya fasihi ya kiapokaliptiki (yaani ufunuo wa mambo ya mwisho) kama tanzu ya kibiblia, ikijumuisha ufafanuzi wake, aina za apokaliptiki katika Biblia (yaani, Danieli na Ufunuo), aina kuu mbili za apokalipsi za Kiyahudi, na kitabu cha apokaliptiki kilicho dhahiri zaidi katika maandiko, yaani kitabu cha Ufunuo. • Kufafanua kanuni tatu za ufasiri wa tanzu za kiunabii na kiapokaliptiki za maandiko: umuhimu wa kuweka mkazo zaidi kwa Yesu Kristo, kuelekeza jumbe za kinabii katika wito wa Ufalme wa Mungu, na kusisitiza juu ya kutimia kwa makusudi makuu ya Mungu hata katika nyakati za uovu, mateso na ukosefu wa haki.
3
Njoo, uchunguze kina cha Neno!
Ibada
Zaburi 78:1-8 – Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu, Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu. 2 Na nifunue kinywa changu kwa mithali, Niyatamke mafumbo ya kale. 3 Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu, Ambayo baba zetu walituambia. 4 Hayo hatutawaficha wana wao, Huku tukiwaambia kizazi kingine, Sifa za Bwana, na nguvu zake, Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya. 5 Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, Na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu Wawajulishe wana wao, 6 Ili kizazi kingine wawe na
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker