Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 1 1 5

K U T A F S I R I B I B L I A

habari, Ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao 7 Wamwekee Mungu tumaini lao. Wala wasiyasahau matendo ya Mungu, Bali wazishike amri zake. 8 Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu. Mungu alikusudia nini hata sehemu kubwa ya Biblia ikaandikwa katika tamathila za usemi, sitiari, taashira (ishara), na hadithi? Kwa nini Mungu atuandikie na kuzungumza nasi kwa njia ya mafumbo na sitiari, na si tu kwa lugha rahisi, iliyonyooka ambayo inaeleweka kwa wepesi zaidi na isiyohitaji kutafsiriwa kwa kina kiasi hiki? Inawezekana kwamba Mungu anajaribu kutupotosha kimakusudi, na kufanya iwe vigumu zaidi kwetu kujua mapenzi yake na Neno lake? Bila shaka hapana! Andiko letu la ibada linaeleza kwa nini Daudi alizungumza kwa mifano na “mafumbo ya kale,” mambo ambayo Mungu aliyafunua kwa watu wake tangu nyakati za kale. Kusudi si kutuficha, kwa kuwa mstari wa nne unaonyesha wazi moja kwa moja kwamba nia ya Mungu si kutuficha maana yake, wala nia yetu haipaswi kuwa kuwaficha watoto wetu maana ya maneno ya Mungu. Badala yake, tumepewa lugha ya picha, mafumbo na hadithi, istiari na ushairi, taashira (ishara) na sitiari ili kutualika kujifunza, kutafiti, kumtafuta Mungu kwa namna itakayosababisha maajabu na kazi zake kueleweka vyema na watu wake na watoto wao. Je, ni kwa namna gani mifano, hadithi, sitiari, au lugha ya picha vinatualika kuja na kuchunguza? Kwanza, kupitia taswira au picha Mungu hutuonyesha kile anacho maanisha badala ya kutuambia tu. Kwa kutuelekeza kwenye maua ya kondeni na jinsi anavyoyatunza, anaweza kutupa picha halisi ya maana ya kutunzwa na yeye. Pili, taswira, hadithi, na picha zinahusisha mawazo na hisia zetu pamoja na akili zetu. Mungu hataki tujue mawazo tu bali tuathiriwe nayo, tuhisi uhalisia. Mwisho, kuwasiliana kupitia mafumbo na hadithi kunawaalika wenye njaa kuendelea kutafuta maana ya utanzu huo. Kupitia taswira, picha, na hadithi Mungu, kimsingi, anatualika kuja na kuchunguza zaidi na zaidi kile anacho maanisha. Kwa wale ambao walikuwa wanatafuta almasi juu ya uso wa maandiko, watakatishwa tamaa. Maandiko kila mahali yanazungumza namna ambavyo moyo wenye njaa huleta matokeo makubwa kwa kule kuchunguza na kutafuta hekima kama hazina ili kupokea ufahamu wake wa ndani na bora zaidi. Mithali 2:1-5 – Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu; 2 Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; 3 Naam, ukiita busara, Na kupaza sauti yako upate ufahamu; 4 Ukiutafuta kama fedha, Na kuutafutia kama hazina iliyositirika; 5 Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana, Na kupata kumjua Mungu.

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker