Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 1 6 /

K U T A F S I R I B I B L I A

1Wafalme 3:9 –Kwa hiyo nipemimi mtumwa wakomoyowa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? Zaburi 25:4-5 – Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako, 5 Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Zaburi 119:34 – Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, Naam, nitaitii kwa moyo wangu wote. Mithali 3:6 – Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Mithali 8:17 – Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. Luka 11:13 – Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? Yakobo 1:5 – Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Kwa kweli hii ndio sababu iliyomfanya Bwana kuzungumza kwa mafumbo. Kwa wale ambao hawakuwa na nia ya kutafuta mapenzi na nia ya Bwana, fumbo lilikuwa kama mwisho wa mazungumzo, neno ambalo halikuwavutia wala kuchochea uchunguzi zaidi. Kwa wale ambao kwa kweli walikuwa na njaa ya kweli, fumbo lilikuwa mwaliko wa kutafuta kile ambacho Bwana alimaanisha, na kuchimba zaidi ili kufahamu mengi kuhusiana na kazi ya Mungu. Kwa wale ambao hawataki kuchunguza mambo, matumizi ya tamathila za usemi yaliwakatisha tamaa na kuwafunga fahamu, kama inavyoonyeshwa katika nukuu za Agano Jipya kuhusu Zaburi ya 78 katika mafundisho ya Bwana Yesu: Mathayo 13:13 – Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. Mathayo 13:34-35 – Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno; 35 ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali. Marko 4:33-34 – Kwa mifano mingi ya namna hii alikuwa akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulisikia; 34 wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha.

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker