Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 1 1 7

K U T A F S I R I B I B L I A

Biblia ni ulimwengu wa tamathila za usemi ambamo kila fumbo, hadithi, taashira, na sitiari inawakilisha mwaliko wa kutafuta na kupambanua nia ya Bwana iliyo katika kweli ya Neno lake. Njoo, ujiunge na safari hii ya kusisimua na utafute kweli ya Bwana katikati ya ulimwengu huu wa tamathila za usemi.

Baada ya kutamka na/au kuimba ukiri huu wa Imani (taz. kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu wa rehema, uliahidi kutovunja agano lako nasi. Katikati ya maneno yote yanayobadilika ya kizazi chetu, sema Neno lako la milele ambalo halibadiliki. Nasi tuitikie ahadi zako za neema kwa kuishi maisha ya uaminifu na utii; kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, Amina.

Kanuni ya Imani ya Nikea na maombi.

~ Presbyterian Church (U.S.A.) and Cumberland Presbyterian Church. The Theology and Worship Ministry Unit. Book of Common Worship . Louisville: Westminister/John Knox Press, 1993. p. 91.

3

Weka kando daftari na matini yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ujibu maswali ya jaribio la Somo la 2, Hemenetiki ya Kibiblia: Mbinu ya Hatua Tatu .

Jaribio

Mazoezi ya kukariri maandiko

Rudia na mwenzako, andika na/au nukuu kifungu cha mstari wa kumbukumbu wa kipindi cha darasa kilichopita: Ezra 7:10; Matendo 17:11; na Zaburi 1:1-3.

Kabidhi muhtasari wako wa kazi za usomaji za juma lililopita, yaani, jibu lako fupi lenye maelezo machache kuhusu mawazo muhimu ambayo waandishi walikusudia kuwasilisha katika vitabu ulivyoagizwa kusoma (Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za kukusanya

MIFANO YA REJEA

Neno ni Neno, sivyo?

Wengi wanaamini kwamba Neno la Mungu halipaswi kuwa gumu kupita kiasi, na kwamba inatosha kupata ile maana iliyo wazi, halisi katika kila kifungu. Wengi wanaoshikilia msimamo huu wanahisi kwamba kuzingatia aina za fasihi na kanuni za kila moja kunaweza kufanya Neno la Mungu lisieleweke na mtu ye yote isipokuwa wale ambao ni wataalamu wa kanuni za fasihi na fasili za tanzu. Sehemu ya kuvutia zaidi ya hoja yao ni pale wanapodai waziwazi kwamba wanaamini katika faida ya Neno la Mungu kwa wote, waamini wachanga, wenye ukomavu kiasi na waliokomaa.

1

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker