Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 2 6 /
K U T A F S I R I B I B L I A
d. Sheria dhidi ya Injili – Kanuni zinazokinzana za namna ya kumkaribia Mungu na kuishi maisha ya Kikristo, Rum. 11:6.
e. Sheria ya Kristo – Gal. 6:2; Yoh. 13:34-35
C. Nyaraka (barua) – Barua zilizoandikwa na mitume kwa makanisa ya Kikristo ili kuhimiza na kuwekea mkazo kweli za Injili, na kutatua changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo katika mazingira na wakati wao.
1. Nyaraka ni “urithi wa kifasihi kwa watu wote” (taz. mifano yake katika Agano la Kale, k.m., 2 Sam. 11; 2 Wafalme 5; Isa. 37).
2. Uwiano kati ya matakwa ya kitheolojia na hitaji binafsi na la jamii ya waaminio.
3
3. Nyaraka za Paulo – Wakorintho, Wagalatia, Wafilipi, Wathesalonike, Waefeso, Wakolosai, Warumi, Waebrania(?), Filemoni, Timotheo, Tito.
4. Nyaraka za Petro - 1 na 2 Petro
5. Nyaraka za Yohana - 1, 2, na 3 Yohana
6. Nyaraka za jumla - Yakobo, Waebrania, Yuda.
Nyaraka zina sifa ya balagha (kuandika kwa hoja), za kibinafsi (zimeandikwa kwa watu wanaojulikana), za kiroho (zinaangazia mada muhimu za kiroho), mafundisho (kushughulika na maswala ya kitheolojia), mahususi (zinalenga kushughulikia mahitaji fulani), na za vitendo (zinazolenga kutoa changamoto na kuwatia moyo waumini katika kutembea kwao na Mungu na waumini wengine).
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker