Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 1 2 7

K U T A F S I R I B I B L I A

D. Unabii – maandiko katika Agano la Kale na Agano Jipya ambayo yanaonyesha kuwa Mungu anao ujuzi na ufahamu wa hali ya juu kuhusu kila nyanja ya maisha yetu (ya zamani, ya sasa, na yajayo), na namna anavyoona mambo yajayo ya ulimwengu huu na hatima yake.

1. Kuhutubu – uwasilishaji wa Neno la Mungu la sasa kwa mtu au watu katika mazingira fulani kwa njia ya maonyo, kutia moyo, na changamoto (k.m., Nathani na Daudi).

2. Kutabiri – uwasilishaji wa mtazamo na maono ya Mungu kwa mtu au watu kuhusu siku zijazo (k.m., Isaya 11).

3. Ofisi ya kinabii na unabii vinapatikana kote katika Maandiko Matakatifu.

3

a. Musa kama nabii wa kielelezo (rej. Kumb. 18:15-19).

b. AK – manabii “wakubwa” na “wadogo”, Sauli, Balaamu.

c. AJ – Kristo, mitume, Anna, Agabo, Kayafa.

4. Tabia za unabii

a. Utajiri wa taashira za kifasihi.

b. Kuingiliana kwa historia na utabiri.

c. Ulilenga zaidi baraka za Mungu za kimaadili au hukumu.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker