Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 1 5 7
K U T A F S I R I B I B L I A
3. Wito wa utakatifu na utauwa tukitarajia hukumu ya haki juu ya mambo yote, 2 Pet. 3:10-14.
C. Kanuni ya Tatu: Sisitiza juu ya kutimia kwa makusudi makuu ya Mungu hata katika nyakati za uovu, mateso na ukosefu wa haki.
1. Utawala wa ufalme wa Mungu hatimaye utaziponda falme zote za dunia, Dan. 2:44.
2. Kusudi kuu la Mungu hatimaye litatimizwa katika nyanja zote za ulimwengu, yote kwa ajili ya utukufu wake na Jina lake, Dan. 4:34-37.
3. Hatimaye Mungu atamlipa kila mwanadamu kwa kadiri ya matendo yake, yawe mema au mabaya, Ufu. 22:8-16.
3
Hitimisho
» Katika somo la tanzu za Biblia, pengine hakuna nyingine zilizo mashuhuri na muhimu kwa ajili ya kujifunza kama simulizi na unabii. » Kwa kugundua kanuni za aina mbalimbali za tanzu katika maandiko, tutapata uwezo wa kuelewa na kutumia kanuni za aina husika ili kuipata kweli ya Mungu katika Neno lake la ajabu.
Maswali yafuatayo yaliundwa ili kukusaidia kupitia maarifa uliyojifunza katika sehemu ya pili ya video. Katika sehemu hii tuliangazia mada ya “hemenetiki maalum” katika aina mbili tofauti za fasihi, yaani simulizi na unabii. Simulizi zinatumika kama msingi wa theolojia ya hadithi, na unabii unawasilisha ukweli kuhusu Mungu na ulimwengu katika njia za kibinafsi na za kifasihi. Kadri unavyoendelea kuwa mahiri zaidi katika kufasiri tanzu, utajengwa na kustawi zaidi kupitia Neno, kadhalika utakua katika uwezo wako wa kufundisha na kuhubiri Neno kwa nguvu na uwazi. Jibu maswali yafuatayo, huku ukipitia kwa umakini
Sehemu ya 2
Maswali kwa wanafunzi na majibu.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker