Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 5 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
dhana kuu kuhusiana na hemenetiki maalum za simulizi na unabii, ikijumuisha fasihi ya apokaliptiki. 1. Toa ufafanuzi wa “hemenetiki maalum,” na eleza namna ambavyo kanuni na taratibu zake zinatusaidi katika kufasiri aina mbalimbali za fasihi za Biblia. 2. Simulizi ni nini, na zina umaarufu gani katika Biblia yenyewe? Kuna tofauti gani kati ya simulizi za “kihistoria” na “za kufikirika?” 3. Wanatheolojia wa simulizi au hadithi wanahusiana vipi na simulizi za maandiko? Taja dhana za jumla ambazo ni msingi wa dhana ya theolojia ya hadithi. 4. Kati ya dhana zote za wanatheolojia wa hadithi, ni ipi (zipi) unaamini ni muhimu zaidi kwa sisi sote ambao tunatafuta kuchukulia hadithi za Biblia kwa uzito kama historia na ufunuo wa Mungu? 5. Je, kuna uhusiano gani kati ya namna tunavyofasiri hadithi na mafafanuzi na maana ambayo Mungu anatupa kupitia maelezo ya mwandishi katika masimulizi ya hadithi za Biblia? Elezea jibu lako. 6. Orodhesha kauli muhimu kuhusu hadithi, Biblia, na Kanisa tulizojifunza katika sehemu hii. Kati ya kauli hizi zote, ni ipi (zipi) unaamini ni muhimu zaidi kwetu kutambua tunapotafuta kuchukulia kwa uzito nafasi ya simulizi katika kutafsiri Biblia? Elezea jibu lako. 7. Ni vipengele gani vya jumla vya masimulizi katika maandiko, na vinahusiana vipi kama vipengele vya hadithi nyingine zinazosimuliwa mahali pengine katika riwaya, hadithi fupi, au aina nyinginezo za fasihi? 8. Eleza maana ya unabii kama tanzu kuu ya maandiko. Ni ukweli gani tunaoujua kuhusu unabii kuhusiana na ujuzi wetu juu ya Mungu, ulimwengu wote mzima, na kazi ya Mungu ulimwenguni? 9. “Fasihi ya apokaliptiki” ni nini, ni vitabu gani vya Biblia yetu ni vya aina hii ndogo ya unabii, na kwa nini elimu ya utanzu wa apokaliptiki ni muhimu sana kwa ufasiri mzuri wa Biblia? 10. Kanuni na mitazamo gani mitatu ni muhimu ikiwa tunataka kutafsiri kwa usahihi tanzu za unabii na apokaliptiki za maandiko?
3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker