Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 6 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
muda mwingi zaidi katika vitabu vya Injili na Matendo ya Mitume, na simulizi nyingine za Biblia? * Katika kuangalia kauli tulizojifunza katika somo hili kuhusiana na theolojia ya hadithi, kuna kauli ambayo unadhani imevuka mipaka ya uhalisia au si ya kweli kwako? Elezea jibu lako. Ikiwa ndivyo, unawezaje kurekebisha kauli hiyo ili iendane zaidi na kile unachoamini? * Umewahi kusoma maandiko ya unabii na apokaliptiki kwa kina? Ni nini kingepaswa kufanyika kabla ya kuanza kujifunza aina hii ya fasihi katika Biblia—una mapungufu gani katika ufahamu wako wa namna ya kujifunza vitabu hivyo? Katika kuangalia utofauti wa nyenzo za kifasihi katika Biblia (yaani, mashairi, nathari, nyimbo, tenzi, hadithi, sitiari, fasihi ya ishara, unabii, istiari, mafumbo, n.k.) wengine hukatishwa tamaa sana na elimu ya tanzu. Sababu ziko dhahiri kabisa! Mtu angeweza kutumia muda kiasi gani hata utoshe kujifunza aina zote za tanzu za Biblia na kuzielewa kwa ufasaha? Kazi ya namna hiyo inawezekana kweli? Hakuna wasomi ambao wametumia miongo kadhaa kujikita katika aina fulani mahususi ya utanzu, na bado wanakiri kwamba hawaielewi vizuri? Sisi ambao si wataalamu wa lugha za kibiblia au tanzu zenyewe, tunawezaje kutumia kanuni hizi kama msingi wa kujifunza kwetu Biblia? Kujifunza Biblia kwa mtazamo huu wa kuzingatia masuala ya tanzu za fasihi na kanuni zake hakutufanyi tu tulemewe na sheria na kanuni nyingi ambazo yatupasa kuzimudu kabla hatujaanza kupata ufahamu mpya unaopatikana katika Neno la Mungu? Wakati wa mahubiri ya watoto katika makanisa mengi ni wakati wa hadithi tu. Hili si kwamba halina faida au umuhimu. Kwa kawaida wakiwa wameshikilia kitu mkononi cha kutumika kama kielelezo katika utangulizi wa mahubiri, watoto kila juma hupewa ufahamuwamapenzi yaMungu kupitia hadithi ambayo imechaguliwa kwa uangalifu ili kushughulikia suala ambalo kwa kawaida linahusiana na namnawatotowanavyopaswa kufikiria, kuongea, kuenenda, au kufanya maamuzi. Hadithi inatoa kielelezo cha Kweli Kuu, yaani lile fundisho la hadithi, ambalo hadithi hutumika kuelezea. Kwa wengi, aina hii ya matumizi ya msingi ya hadithi ndio matumizi yake yaliyokusudiwa na ya moja kwa moja. Kusema kweli, wengi wanaamini kwamba hadithi ni kwa ajili ya watoto, hasa kwa matumizi ya Shule ya Jumapili ya watoto, mahubiri ya watoto, Kanuni ni nyingi sana! Hadithi ni kwa ajili ya mahubiri ya watoto!
MIFANO
1
3
2
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker