Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 1 6 3

K U T A F S I R I B I B L I A

au shule ya Biblia wakati wa likizo. Msingi wa mtazamo huu ni dhana ya kwamba hadithi ni aina ya msingi na rahisi zaidi ya uwasilishaji wa kweli za kidini, na kwamba fundisho (doktrini) ni namna ya kujifunza maandiko kwa kina cha ndani zaidi, kwa uwazi zaidi, na inayowafaa watu wazima zaidi. Mtazamo huu unapingwa kwa nguvu kubwa na makundi mengi ya Wakristo. Wanatheolojia wa hadithi na simulizi leo wanasisitiza kwamba hadithi ndicho chombo cha msingi na muhimu zaidi cha kuwasilisha kweli ya Mungu, kama ambavyo maandiko yanamwonyesha Bwana wetu mwenyewe akitumia mafumbo, sitiari na lugha ya picha katika mafundisho yake. Kwa mtazamo wako, nani yuko sahihi, wale wanaoamini kwamba hadithi kimsingi ni kwa ajili ya mahubiri ya watoto, au wale wanaoamini kwamba hadithi ni sehemu ya msingi na muhimu zaidi katika Neno la Mungu lililoandikwa? Mojawapo ya mbinu muhimu za homiletiki (elimu ya kutunga hotuba) zinazofundishwa katika seminari kila mahali ni “kanuni ya tatu” – mambo matatu, dhana tatu, mawaidha matatu – ya kusaidia kupanga mahubiri na masomo yetu na kufundisha. Njia hii haijakusudiwa kutumiwa pasipo kufikiri kama sheria ya Umedi na Uhajemi, hata hivyo inaelekea kupunguza uwasilishaji kwa namna ambayo mnenaji anabakiwa na mambo machache yaliyo wazi, akitumia maandiko kama rejea kwa kila kipengele na kukikazia kwa kutumia mfano vitendo au kielelezo kutokana na uzoefu. Wachache wangekubaliana na wazo la kwamba kimsingi mahubiri na mafundisho yote yanapaswa kuhusisha ujuzi na ustadi wa kusimulia hadithi, iwe Hadithi ya Mungu katika maandiko yenye kilele chake katika hadithi ya Yesu wa Nazareti, au kusimulia hadithi za watu tunaowajua na mambo ya maisha yetu ya kila siku. Ikiwa ungekuwa katika nafasi ya kufundisha kizazi kipya cha wahubiri na walimu wa kisasa kuhusu mbinu ya mawasiliano ambayo unaamini ingefaa kwa ajili ya huduma mijini, ungewafundisha mbinu gani? Je, ungetilia mkazo zaidi kwa wahutubu hao kujifunza, kuhubiri, na kufundisha kwa njia ya kusimulia hadithi, au ungetilia mkazo zaidi mbinu za homiletiki na mafundisho zilizozoeleka, yaani “mambo matatu, shairi, na maombi”? Mambo matatu, shairi, na maombi?

3

3

Kuumwa na “mdudu wa unabii”.

Wakristo wengi leo hawana ufahamu kuhusu tanzu ya unabii. Mojawapo ya sehemu zinazopuuzwa zaidi za Neno la Mungu, ambazo wahubiri na walimu wengi leo huepuka kuzitumia ni maandiko ya kinabii. Hawaifundishi kwa utaratibu unaoeleweka katika mahubiri yao, wanaipuuza katika vitengo vyao vya Shule ya Jumapili, na kuepuka kuitumia katika harakati za kueneza Habari Njema,

4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker