Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 6 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

yaani uinjilisti. Uwanja wa fasihi ya kinabii mara nyingi unavamiwa na waalimu huria ambao, wakiwa wamebeba gazeti katika mkono mmoja na maandiko ya kinabii katika mkono mwingine, hufanya utabiri juu ya matukio yanayoendelea ulimwenguni na kutumia andiko la unabii kama rejea kuthibitisha utabiri wao. Kwa sababu ya mielekeo hiyo, waamini wengi hukua kiroho pasipokuwa ufahamu sahihi wa kutafakari maandiko ya kinabii na uzoefu wa kuyatafakari. Ni aina gani za mabadiliko tunayopaswa kufanya katika mtazamo, mtindo, na ratiba ili tuweze kweli kukumbatia na kutumia kwa halali maandiko ya kinabii katika makanisa yetu? Kwa nini tafsiri mpya na ya neno la unabii inaweza kufanyika ugunduzi muhimu na wenye nguvu katika mienendo ya kiroho ya makanisa ya mijini? Neno “tanzu” linarejelea muundo fulani maalum wa fasihi ambao hutumika kuwasilisha ukweli, na lazima utafsiriwe kulingana na kanuni za muundo huo. Elimu kuhusu tanzu huanza na mawazo ya kuitazama Biblia kama fasihi, iliyopangiliwa na kutawaliwa na sheria na kanuni kama ilivyo kwa vitabu vingine vya fasihi. Sheria hizo ndizo ambazo Mungu alitumia ili kuwasilisha Neno lake kwetu. Kuna aina na miundo mingi muhimu ya fasihi katika maandiko. Hizi ni pamoja na matumizi ya simulizi (za kihistoria na za kutunga), Sheria (maandiko ya kisheria), nyaraka (barua), unabii, fasihi ya hekima (methali, monolojia, vitendawili, hekaya, mafumbo, istiari, n.k.), na uwepo wa kazi za kishairi. Tanzu hushughulika na mahitaji mahususi ya hadhira husika, hukuza uelewa wetu wa msingi wa masuala ya maisha mwanadamu, hutuwezesha kuufahamu ukweli kwa kuuona ukiwasilishwa katika muundo wake halisi, na pia kuonyesha ustadi wa waandishi wa Biblia kama walivyoongozwa na Roho, na kufunua utajiri wa siri ya Mungu na kazi yake katika dunia. Hemenetiki maalum inarejelea zile kanuni na taratibu mahususi zinazotuwezesha kufasiri aina za kifasihi za Biblia. Simulizi, aina inayotawala zaidi katika maandiko, hushughulikia mada ambayo ni ya kihistoria (iliyotokea katika maisha halisi) au ya kubuniwa. Wanatheolojia wa hadithi wanatazama hadithi kama njia kuu ya Mungu ya kufunua asili yake na kazi yake katika maandiko, na wanasisitiza kwamba theolojia katika ujumla wake ni tafakuri ya hadithi za Biblia, ambazo kihistoria ni za kuaminika na sahihi, na zinaonyesha ufundi na ujuzi wa waandishi, na kile ambacho Bwana alimaanisha katika maelezo yake mwenyewe kuhusiana na hadithi hizo. Theolojia simulizi inathibitisha kwamba hadithi hutuleta katika uwepo wa kisakramenti, ni muhimu zaidi kuliko maelezo ya kawaida, na zinakubalika katika jamii ya Kikristo. Mapokeo ya Kikristo hubadilika na kujifafanua yenyewe kupitia hadithi, ambazo pia hutangulia na kuzaa jumuiya, maonyo na uwajibikaji, na huzaa theolojia, liturjia na sakramenti. Kama fasihi nyingine, vipengele vya jumla vya simulizi katika

Mapitio ya Tasnifu ya Somo

3

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker