Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 1 6 5

K U T A F S I R I B I B L I A

maandiko ni pamoja na mazingira, wahusika, mtazamo wa mwandishi, mtiririko (ploti), na dhamira ya hadithi. Unabii kama moja ya tanzu kuu za maandiko, ni aina ya fasihi inayoshughulika na Mungu na uhusiano wake na watu wake, mataifa, na uumbaji. Apokaliptiki ni aina ndogo au tawi la unabii, na inajumuisha aina mbili kuu za apokalipsi za Kiyahudi: kitabu cha Agano la Kale cha Danieli na kitabu cha apokaliptiki dhahiri zaidi katika maandiko, yaani kitabu cha Ufunuo. Kanuni tatu pana zaweza kutusaidia kufasiri tanzu za kinabii na za kiapokaliptiki kwa njia ifaayo: kuweka mkazo zaidi kumhusu Yesu Kristo, kuelekeza jumbe za kinabii kwenye mwito wa Ufalme wa Mungu, na kusisitiza juu ya kutimia kwa makusudi makuu ya Mungu hata katika nyakati za uovu, mateso na ukosefu wa haki. Ikiwa una nia ya kujifunza kwa kina zaidi ya mawazo yaliyomo katika somo hili la Fasihi ya Kibiblia: Kutafsiri tanzu za Biblia , unaweza kusoma vitabu vifuatavyo: Adler, Mortimer, and Charles Van Doren. How to Read a Book . New York: Simon and Schuster, 1972. Ryken, Leland. Words of Delight: A Literary Introduction to the Bible . 2nd ed. Grand Rapids: Baker Book House, 1992. ------. How to Read the Bible as Literature . Grand Rapids: Zondervan, 1984. Kuichukulia Biblia kama fasihi kunaweza kufanya maajabu katika kila nyanja ya mahubiri yako, mafundisho, uwasilishaji wako Neno la Mungu. Sio tu kwamba utaanza kuona mambo ambayo kwa kawaida ungeshindwa kuyaona katika jitihada zako za kujifunza Biblia, lakini pia taswira ya ulimwengu wa maandiko itaamsha mawazo yako kwa namna ambayo utaweza kugundua tena “lugha ya asili” ya Biblia. Badala ya kuzingatia tu mawazo, dhana, na mapendekezo, utaanza kuishi katika ulimwengu wa tafakuri, simulizi na imani, na hili litakuwezesha “kutanua mbawa zako” kwa namna ambayo utaeneza habari za Kristo katika viwango mbalimbali vya huduma yako, nyumbani, kazini, na kupitia kanisa lako. Jiweke wazi na tayari kwa njia ambazo Roho Mtakatifu anaweza kutaka ujumuishe mbinu hizi katika kila nyanja ya ushuhudiaji wako na huduma yako, na utumie muda mzuri wiki hii kutafakari juu ya nguvu ya fikra na simulizi katika maisha na kazi yako. Unapofikiria kuhusu kazi yako ya huduma kwa ajili ya kukamilisha moduli hii, unaweza kuitumia ili kukuza ufahamu wako kuhusu kweli hizi kwa njia ya vitendo.

Nyenzo na bibliografia

3

Kuhusianisha somo na huduma

Tafuta uso wa Bwana kwa habari ya ufahamu wako mwenyewe na matumizi ya kanuni zinazohusiana na tanzu katika kutafsiri Biblia, na usisite kupata mtu wa

Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker