Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 6 6 /
K U T A F S I R I B I B L I A
kushirikiana naye katika maombi ambaye anaweza kushiriki kukuombea kwa mzigo na kuinua maombi yako kwa Mungu. Pata ushauri na maelekezo kwa mwalimu wako unapoendelea kuchimbua na kufanyia kazi ujuzi na na maarifa uliyoyapata kutokana na masomo haya katika maisha yako na jitihada zako binafsi za kujifunza. Zaidi ya yote, mruhusu Bwana akuongoze katika njia mpya, na uwaombe wenzako wakuombee anapokuongoza katika mwelekeo mpya katika kujifunza kwako mwenyewe na kuliweka Neno la Mungu katika vitendo.
KAZI
2 Timotheo 3:14-17
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi kijacho, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.
Kazi ya usomaji
Kama kawaida unapaswa kuja na Fomu ya Ripoti ya Usomaji yenye muhtasari wako wa kazi za usomaji za wiki. Pia, ni muhimu sasa uwe umechagua andiko kwa ajili ya kazi ya ufafanuzi, na ukabidhi pendekezo lako kwa ajili ya kazi ya huduma.
3
Kazi nyingine
Katika somo hili tumechunguza asili ya elimu ya tanzu katika ufasiri wa Biblia. Tuliona jinsi ambavyo elimu kama hii inatambua aina mbalimbali za matini zinazounda fasihi ya Biblia, na tukasisitiza kwamba tanzu hizi lazima zifasiriwe kulingana na kanuni za fasihi yenyewe. Elimu ya tanzu huanza na dhana fulani kuhusu Biblia kama fasihi, iliyopangiliwa na kutawaliwa na sheria na kanuni kama ilivyo kwa vitabu vingine vya fasihi. Sheria hizi ndizo ambazo Mungu alitumia ili kuwasilisha Neno lake kwetu. Tuliangalia hasa simulizi na unabii, na kuona namna ambayo kuzingatia kwa umakini kanuni fulani kunavyoweza kukuza mtazamo wetu na ufahamu wetu wa msingi juu ya maisha mwanadamu, na kufunua utajiri wa siri ya Mungu na kazi yake ulimwenguni. Katika somo letu linalofuata, tutahitimisha moduli hii kwa kuangalia jukumu la zana na nyenzo za kitaalamu tunapojaribu kuelewa maana ya matini. Zana nyingi za ajabu zilizoandikwa katika nakala mango na za kidijitali zipo ili kuboresha kujifunza kwa mtu yeyote anayetamani kuwa mwanafunzi wa Neno la Mungu, na katika somo letu linalofuata tutajadili upatikanaji, madhumuni, na manufaa ya zana hizi katika ufasiri mzuri wa kibiblia.
Kuelekea somo linalofuata
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker