Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
1 7 4 /
K U T A F S I R I B I B L I A
fasihi. Hawawezi kupata kamusi mpya za lugha au za Biblia za hivi karibuni zaidi. Wameamua kuegemea kwenye wazo la kujinyenyekeza na kuwa wazi kwa Roho Mtakatifu ili kuwasaidia kuelewa Neno la Mungu, na wamejisalimisha kwa furaha kwa uongozi wa mchungaji wao wa kanisa anapokuwa akilihudumia Neno katikati yao. Je, aina hii ya matumizi ya maandiko iliyo wazi, ya unyenyekevu na ya kujitoa kwa dhati haitoshi kwa kiongozi wa Kikristo pia? Kuwekea mkazo umuhimu wa zana na nyenzo hizo hakufanyi jitihada zetu za kufasiri Biblia zitegemee uwezo wetu wa kupata zana ambazo ni ghali sana na ambazo mamilioni ya watu hawawezi kuzipata, achilia mbali kuzielewa? Ni yapi basi basi manufaa ya zana za kitaalamu katika ufasiri wa Biblia, na tunawezaje kuzitumia kwa namna ifaayo? Ingawa zana za usomi na za kitaalamu zinaweza kuongeza uwezo wetu wa kuelewa maneno mengi magumu ya maandiko, ni lazima tujiulize ikiwa zana zina umuhimu sawa na karama hai za Roho Mtakatifu ndani ya Kanisa katika kugundua maana ya Neno la Mungu. Kwa Wakristo wengi wa Kiprotestanti leo, Biblia ni kitabu cha kibinafsi, kitabu kwa ajili ya matumizi binafsi ya kujifunza na ibada. Mara nyingi Wakristowanaichukulia Biblia kamaNeno lisilohusiana kabisa na karama na Kanisa. Hawawategemei sana wanaume na wanawake wenye vipawa katika makanisa yao, lakini huchagua zana, nyenzo, na marejeo ambayo kimsingi yanafundisha kile wanachokifahamu tayari na kukiamini. Pia ni jambo la kawaida kuwasikia waalimu katika jamii ambao wanajikita zaidi kufundisha aina za masomo na tafsiri ambazo tunaziamini tayari, na hivyo tunakuwa wataalamu wa kile ambacho “X” au “Y” anasema kuhusu wokovu, ukombozi, uponyaji, au somo lolote ambalo ni la “moto” wakati huo. Baadhi ya watu wanaozingatia zaidi tafsiri zinazotolewa na mamlaka rasmi ya kanisa wamefika mahala pa kuamini kwamba matumizi ya zana ambazo hazijahakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka ya kichungaji ya kanisa yanaweza kuchochea migawanyiko, mafarakano na hata uzushi. Wanasisitiza kwamba ikiwa kila mkristo anayo mamlaka yake mwenyewe ya kufasiri, tunawezaje kupata maana halisi ya imani ya Kikristo? Je, unafanya nini kuhusu matumizi ya zana na suala zima la kutambua nafasi ya waalimu wenye vipawa rasmi katika kanisa au jamii ya waaminio? Ni nini kinachofaa zaidi—kujifunza kibinafsi au nafasi zetu katika makusanyiko yetu? Matumizi binafsi ya zana na Karama rasmi za ualimu ndani ya kanisa.
2
4
Tafsiri za kisasa zimeharibiwa!
Hata katika siku zetu ambapo tunaweza kupata tafsiri nyingi za kutegemeka zinazotokana na vyanzo vya kale na bora zaidi vya Maandiko Matakatifu tulivyo
3
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker