Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 7 6 /

K U T A F S I R I B I B L I A

• Madhumuni matatu ya kutumia zana za kitaalamu katika ufasiri wa Biblia ni uwezo wa zana hizo wa kutusaidia kuziba mapengo mbalimbali kati ya ulimwengu wa Biblia na ulimwengu wetu wa sasa, uwezo wake wa kutuelekeza kwenye hazina kubwa ya zana bora zilizopo katika siku zetu, na thamani ya zana hizo katika kutusaidia kuwa waaminifu zaidi kwa Neno la Mungu kwa kutuwezesha kugundua kwa upya maana za maandiko katika muktadha wake wa asili. • Ufunguo wa kuelewa zana mbalimbali za ufasiri wa Biblia ni kutambua jinsi gani na kwa njia gani nyenzo fulani inaweza kutusaidia kuziba ombwe la ufahamu kati ya utamaduni wetu na ule wa waandishi wa Biblia na hadhira yao. • Zana za msingi za ufasiri wa Biblia ni pamoja na tafsiri nzuri ya Biblia, kamusi za Kiyunani na ya Kiebrania zilizowekwa kwenye mfumo wa nambari wa Strong , kamusi thabiti ya Biblia, konkodansi, na vitabu vinavyoaminika vya ufafanuzi wa kieksejesia ambao unazingatia zaidi kutoa maana ya kibiblia ya kifungu husika. • Biblia iliandikwa katika lugha tatu (Kiebrania, Kiaramu, na Kiyunani), kwa sababu hiyo tunahitaji tafsiri nzuri ya maandiko katika lugha yetu ya asili. Kwa sababu ya tofauti za lugha, maana ya neno na sarufi, tofauti za kitamaduni na umbali wa kihistoria, na mitazamo na falsafa tofauti miongozi mwa watafsiri, tafsiri hutofautiana sana. • Nyingi za tafsiri zetu za kisasa zinatokana namatini na data zilizothibitishwa na kuhakikiwa, zimerekodiwa vyema na kufanyiwa utafiti thabiti, na zinafaa kutegemewa na mwanafunzi wa Biblia. • Miongoni mwa zana za msingi, konkodansi huorodhesha maneno yote ya Biblia na mahali yanapopatikana kwa mpangilio wa alfabeti, na leksimu hutoa ufafanuzi (matumizi) ya maneno kama yalivyotolewa katika mstari fulani wa maandiko. Kamusi za ufafanuzi huongeza maoni kuelezea uhusiano kati ya maana ya maneno na mafundisho ya kibiblia. • Kamusi za Biblia huorodhesha habari za kihistoria, kijiografia, kiutamaduni, kisayansi, na kitheolojia kuhusu watu, mahali, wanyama, matukio, na vitu halisi vinavyopatikana katika Biblia, na pia muhtasari wa kila kitabu cha Biblia. • Vitabu vya ufafanuzi wa kieksejesia huelezea maoni ya kitaalamu kuhusu maana halisi ya maneno katika matini asilia, ikijumuisha masuala ya sarufi, maana zamaneno, namatokeo ya uhakiki wa Biblia. Pia zinajumuisha taarifa kuhusu ukweli wa kihistoria na maarifa ya kiutamaduni ya ulimwengu wa nyakati za Biblia ambayo yanaweza kuathiri tafsiri ya maandiko.

4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker