Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 8 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

4. Wafasiri hutumia aina mbalimbali za lugha na mitindo katika tafsiri zao.

a. Wanatumia lahaja mbalimbali. (1) Waingereza - KJV, Jerusalem Bible, J.B. Phillips (2) Marekani - RSV, NASB (3) Mchanganyiko - NIV b. Wanatumia mitindo tofauti ya lugha . (1) Mitindo rasmi : KJV, NKJV, RSV (2) Mitindo rasmi ya wastani : NIV, NRSV, TEV (3) Mitindo isiyo rasmi : Phillips, LB, CEV

c. Zipo kesi maalum pia. (1) Biblia za Fasili (paraphrases) . Biblia za Fasili ni matoleo ya Biblia ambayo hayajatafsiriwa kutoka katika lugha asilia. Badala yake tafsiri iliyopo imebadilishwa maneno ili kujaribu kuifanya iwe wazi zaidi au ieleweke zaidi. (2) Toleo la Amplified . Toleo la “Amplified” hutoa maana nyingi iwezekanavyo kwa maneno muhimu yaliyotumiwa katika maandiko. (3) Tafsiri ya Kiyahudi (Jewish Translation). Katika karne ya 20 baadhi ya tafsiri muhimu sana za Biblia za Kiyahudi zilichapishwa. The Holy Scriptures according to the Masoretic Text: A New Translation , na The Complete Jewish Bible ..

4

D. Kuchagua tafsiri nzuri

1. Msingi thabiti wa usomi kwa tafsiri za kisasa . Uvumbuzi mwingi wa matini za kale katika nyakati zetu umethibitisha jinsi ambavyo maandiko

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker