Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 1 8 5
K U T A F S I R I B I B L I A
yetu yaliyotafsiriwa yana sifa za kuaminika, na umetusaidia kuelewa vyema baadhi ya vifungu ambavyo hapo awali vilikuwa vigumu.
a. Hati za Bahari ya Chumvi zilizogunduliwa katika miaka ya 1940 na 1950 zinatupa maandiko ya Agano la Kale ya kabla ya mwaka wa 70 B.K. Hiyo ni zamani zaidi kwa takriban miaka 1000 kuliko maandiko yoyote tuliyokuwa nayo kabla ya wakati huo.
b. Mnamo mwaka 1898, hati mpya 35 za Agano Jipya zilipatikana huko Misri. Katika karne ya 20, karibu hati 100 zenye sehemu za Agano Jipya zimegunduliwa.
2. Misingi bora ya kielimu ndio msingi wa kazi ya tafsiri zetu za kisasa.
3. Tafsiri nyingi leo zimerekodiwa vizuri, zimefanyiwa utafiti, na zinategemeka.
4
4. Chagua tafsiri na uifahamu. Yoyote kati ya zifuatazo inatatumika kama tafsiri ya msingi inayotegemeka katika kujifunza Biblia .
a. English Standard Version - ESV
b. New King James Version (or King James Version) - NKJV or KJV
c. New International Version - NIV
d. New Revised Standard Version (or Revised Standard Version) - NRSV or RSV
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker