Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

1 9 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

• Visaidizi vya rejea mtambuka ( cross-references ) vinaangazia uhusiano wa matini na vifungu mbalimbali ambavyo vinazungumzia mada moja au vina kiini kimoja cha mada katika ufafanuzi wa Biblia (k.m., Biblia za mada, Biblia za rejea mtambuka, na miongozo ya mada na konkodansi). Ingawa haya yanatusaidia kuhusianisha maandiko katika somo fulani, ni lazima tuwe waangalifu tusifanye makosa ya muktadha tunapounganisha aya, na tukumbuke kila mara kwamba wahariri wanaweza kuhusianisha vifungu kwa namna isiyo halali na isiyoweza kutetewa. • Zana fulani hutoa usuli wa historia, utamaduni, desturi za kijamii, watu, na mazingira ya kijiografia ya ulimwengu wa Biblia. Hizi ni pamoja na kamusi za Biblia, ensaiklopidia za Biblia, atlasi za Biblia na vitabu vya mwongozo, na kazi zinazohusu historia na desturi za Biblia. Zana hizi zinaweza kutoa kiasi cha kushangaza cha taarifa juu ya ulimwengu wa maandiko, lakini lazima zisomwe kwa uangalifu ili kutofautisha data ya kihistoria na tafsiri inayohusu uhalali wa maandiko yenyewe . • Zana nyingine ni muhimu hasa kwa ajili ya kupata taarifa za usuli juu ya mwandishi, tarehe, na hali au mazingira ya kitabu, na matumizi fulani maalum ya lugha katika ufasiri na ufafanuzi (taashira, sitiari, lugha ya kitamathali, n.k.). Zana hizi ni pamoja na vitabu vya miongozo ya Biblia, Biblia za kujifunzia, na miongozo ya taswira za Biblia. Tunapaswa kuwa waangalifu katika kupima maoni yaliyomo katika nyenzo hizi tukijua kwamba ni mitazamo na mawazo ya waandishi wenyewe na sio maandiko yenyewe . • Vitabu vya ufafanuzi ni visaidizi vya kutusaidia kufasiri maana ya kitabu fulani cha maandiko katika mtazamo wa mchungaji fulani, msomi fulani, au mfasiri fulani wa Biblia. Kuna aina nne kuu za vitabu vya ufafanuzi kama visaidizi katika kujifunza kwetu: vitabu vya ibada, mafundisho, ufafanuzi, na homiletiki (yaani, visaidizi vilivyoundwa mahususi kwa ajili wahubiri na walimu kutoa mahubiri na kuandaa masomo ya Biblia). Ingawa vitabu vya ufafanuzi vinaweza kuongeza maarifa yetu juu ya maandiko, havipaswi kamwe kufanyika mbadala wa jitihada zetu binafsi za kujifunza maandiko yenyewe. • Matumizi sahihi ya zana hizi za msingi na za ziada ni yale yanayolenga kutusaidia kuziba pengo kati ya dunia hizi mbili: ulimwengu wa maandiko na ulimwengu wetu wa sasa. Hakuna maelezo au dhana kutoka kwa mfasiri yeyote inayopaswa kukubaliwa endapo itakanusha au kupinga ushuhuda wa maandiko yenyewe. Hakuna chochote katika zana yoyote kitakachokubaliwa ikiwa kitaonekana kupingana na fundisho lililo wazi la maandiko kuhusiana na Kristo na kazi yake ya ukombozi kwa njia ya msalaba.

4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker