Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 2 5 9
K U T A F S I R I B I B L I A
Tamathali za Semi (muendelezo)
yanawakilisha namna anavyo ona vitu, au mtazamo wake wa akili. Na, “. . . Bali ulimi wa mwenye haki ni afya ” (Mit. 12:18) ambapo ulimi unaosimama kwa kile ambacho mwenye haki anasema, maneno yake ni hekima. Katika Agano la Jipya, “ndipo walipomwendea Yerusalemu na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani. . .” (Mt. 3:5) ambapo ni dhahiri kwamba waliotajwa hapa ni watu sio maeneo ya kijiografia. Kisha, tuna tazama “hauwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani” (1 Kor. 10:21). Hata kikombe na meza vinatumika kutokana na vile ambavyo vinabeba na vile ambavyo vinatoa. Tena, katika Warumi 3:30, tohara inatumika kuwakilisha Wayahudi wakati wasiotahiriwa wanawakilisha watu wa mataifa. Nina uhakika kutokana na mifano hii utakuwa umeona namna taashira inavyotumika katika Biblia. Tunatumia mfano huohuo leo pale tunapomuita mtu “simba-marara” au “paka.” Kutengeneza picha iliyokubwa zaidi ya uhalisia kwa kuikuza makusudi iwe zaidi ya ukweli ni kawaida kabisa katika mazungumzo yetu, hivyo chuku (kukuza zaidi) lazima iwe ile inayojulikana kwetu. Katika uchungu wa mateso yake, Ayubu anaingiza aina hii ya lugha. Kwa namna ya picha zaidi kuliko aina yoyote nyingine ya mazungumzo, inaonyesha kutisha kwa hisia zake za mateso. Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu; siku za mateso zimenishika. Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu, na maumivu yanayonitafuna hayapumziki. Kwa ugonjwa wangu Kuwa na nguvu nyingi mavazi yangu yameharibika; hunikaza kama shingo ya kanzu yangu. Yeye amenibwaga topeni, nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. Chuku
Nakulilia wewe, wala huniitikii; Nasimama, nawe wanitazama tu. Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu; nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker